4- Kutoa damu kutoka mwilini kwa kufanyiwa chuku au kujitolea kuchotwa damu ili aweze kumpa mgonjwa. Yote hayo yanamfunguza.

Kuhusu kutolewa damu kidogo – kama ile inayotolewa kwa ajili ya kipimo –  hii haiathiri funga yake. Vivyo hivyo kutokwa na damu pasi na kutaka kwake – kama kutokwa na damu puani, katika donda au kung´oa jino – ni mambo yasiyoathiri swawm.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Mulakhasw al-Fiqh (01/384)
  • Imechapishwa: 24/04/2021