Haafidhw Abul-Qaasim at-Twabaraaniy amesema katika kitabu ”Kitaab-us-Sunnah”:

“Mlango unaozungumzia kulingana kwa Allaah (Ta´ala) juu ya ´Arshi Yake hali ya kutengana na viumbe Wake.”

Kisha akasimulia Hadiyth ya kondoo na kwamba ´Arshi ipo juu ya migongo yao na kwamba Allaah yuko juu yake na akataja mambo mengine yanayohusiana na hilo.

Abul-Hasan ´Aliy bin Mahdiy at-Twabariy, ambaye ni swahiba yake al-Ash´ariy, amesema:

“Tambua ya kwamba Allaah (Subhaanah) yuko juu ya mbingu, juu ya kila kitu, amelingana juu ya ´Arshi Yake, kwa maana kuwa yuko juu yake. Maana ya kulingana ni kupaa, kama wanavyosema waarabu: ”Nimepanda juu ya mgongo wa mnyama, ”Nimepanda juu ya dari”, ”Jua limekuwa juu ya kichwa changu” na kwamba ”Ndege amesimama juu ya kilele cha kichwa changu” kwa maana kuwa limepaa hewani hadi likawa juu ya kichwa changu. Hivyo basi wa Milele (´Azza wa Jall) yuko juu ya ´Arshi Yake kwa namna ya kwamba yuko juu ya mbingu na juu ya ´Arshi Yake. Amesema (Ta´ala):

أَأَمِنتُم مَّن فِي السَّمَاءِ أَن يَخْسِفَ بِكُمُ الْأَرْضَ فَإِذَا هِيَ تَمُورُ

“Je, mnadhani mko katika amani na aliyeko juu mbinguni kwamba hatokudidimizeni ardhini, tahamaki hiyo inatikisika?”[1]

يَا عِيسَى إِنِّي مُتَوَفِّيكَ وَرَافِعُكَ إِلَيَّ

“Ee ‘Iysaa! Hakika Mimi ni Mwenye kukuchukua na Mwenye kukupandisha Kwangu.”[2]

إِلَيْهِ يَصْعَدُ الْكَلِمُ الطَّيِّبُ وَالْعَمَلُ الصَّالِحُ يَرْفَعُهُ

“Kwake linapanda neno zuri na tendo zuri hulitukuza.”[3]

يُدَبِّرُ الْأَمْرَ مِنَ السَّمَاءِ إِلَى الْأَرْضِ ثُمَّ يَعْرُجُ إِلَيْهِ فِي يَوْمٍ كَانَ مِقْدَارُهُ أَلْفَ سَنَةٍ مِّمَّا تَعُدُّونَ

”Anayaendesha mambo kutoka mbinguni mpaka ardhini, kisha inapanda Kwake katika siku ambayo kipimo chake ni sawa na miaka elfu katika yale mnayoihesabu nyinyi.”[4]

Haafidhw Abu Bakr Ahmad bin Ibraahiym bin Shaadhaan amesema: Bwana mmoja ninayemwamini, na ambaye mwanangu pia Abu ´Aliy alimsikia, amenisimulia:

”Tulikuwa tunamuosha maiti ambaye alikuwa amelala juu ya kitanda chake. Wakatu tulipomvua nguo tukamsikia anasema: ”Yuko juu ya ´Arshi Yake peke Yake. Yuko juu ya ´Arshi Yake peke Yake.” Tukatawanyika kutokana na woga wa maneno hayo makubwa tuliyoyasikia. Kisha tukarudi tukamwosha.”

Ameyapokea Imaam Muwaffaq-ud-Diyn i ”Ithbaatu Swifat-il-´Uluww”.

Imaam na Haafidhw Abul-Hasan ad-Daaraqutwniy (Rahimahu Allaah) amesema:

Hadiyth ya uombezi ya Mteule Ahmad

iko kwa Ahmad tumeipokea kwa cheni ya wapokezi iliyoungana

Kuhusu Hadiyth ya ukaaji juu ya ´Arshi,

hatuikanushi pia

Ipitisheni Hadiyth kama ilivyo

na msiingizie mambo yanayoiharibu

Msipinge kuwa ataketi

wala msikanushe kuwa Atamketisha

[1] 67:16-17

[2] 3:55

[3] 35:10

[4] 32:5

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Ahmad bin ´Abdil-Haadiy al-Maqdisiy (afk. 744)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Kalaam ´alaa Mas-alat-il-Istiwaa’ ´alaal-´Arsh, uk. 74-76
  • Imechapishwa: 29/12/2025