20. Haifai kukusanya kabla mtu hajaanza safari

Swali 20: Kuna mtu alitaka kusafiri baada ya swalah ya Dhuhr na kabla ya kuingia wakati wa swalah ya ´Aswr – je, inafaa kwake kukusanya kati ya Dhuhr na ´Aswr katika wakati wa swalah ya Dhuhr[1]?

Jibu: Haifai kwake kukusanya kati ya swalah mbili mpaka pale atapoyaacha majengo ya mji wake au akaanza kuona jangwa. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliswali Dhuhr mwaka wa hajj ya kuaga Madiynah Rak´ah nne kisha akatoka na kuswali ´Aswr Dhul-Hulayfah Rak´ah mbili.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (10/286).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Musaafir, uk. 36
  • Imechapishwa: 03/03/2022