82 – Abu ´Abdillaah Muhammad bin Ahmad bin Muhammad bin Ahmad bin Abiy Twaahir ad-Daqqaaq na Abul-Qaasim ´Abdur-Rahmaan bin ´Ubaydillaah bin Muhammad bin al-Husayn al-Jarmiy wametukhabarisha: Abul-Hasan ´Aliy bin Muhammad bin az-Zubayr al-Kuufiy ametukhabarisha: al-Hasan bin ´Aliy bin ´Affaan al-´Aamiriy ametuhadithia: Zayd bin al-Hubaab ametuhadithia, kutoka kwa Maalik bin Mighwal: Nimemsikia ash-Sha´biy akisema:

”Natamani laiti nisingekuwa nimejifunza chochote katika elimu.”

83 – Abu Bakr Muhammad bin ´Abdillaah bin Abaan ath-Tha´labiy ametukhabarisha: Abu Bakr Ahmad bin Salmaan an-Najjaad ametuhadithia: Ahmad bin Muhammad bin Shaahiyn ametuhadithia: Ibn Sahl – yaani Muhammad bin Sahl bin ´Askar – ametuhadithia: Nimemsikia al-Firyaabiy akisema: Nimemsikia Sufyaan ath-Thawriy akisema:

”Natamani laiti nisingelikuwa nimeandika elimu. Natamani laiti ningelisalimishwa na elimu, na isiwe ni hoja kwangu wala hoja dhidi yangu.”

84 – Abul-Qaasim Twalhah bin ´Aliy bin as-Saqr al-Kattaaniy ametukhabarisha: Abu Bakr Muhammad bin ´Abdillaah bin Ibraahiym ash-Shaafi´iy ametukhabarisha: Abu ´Iysaa Muusa bin Haaruun at-Twuusiy ametuhadithia: Abu Ma´mar ametuhadithia: Nimemsikia Ibn ´Uyaynah akisema:

”Elimu isipokunufaisha basi itakudhuru.”

Bi maana isipokunufaisha kwa wewe kuitendea kazi, basi itakudhuru kwa njia ya kwamba itakuwa ni hoja dhidi yako.”

85 – Abu ´Aliy al-Hasan bin ´Aliy bin Muhammad at-Tamiymiy ametukhabarisha: Abu Bakr Ahmad bin Ja´far bin Hamdaan bin Maalik al-Qatwiy´iy ametukhabarisha: ´Abdullaah bin Ahmad bin Hanbal ametuhadithia: Baba yangu amenihadithia: Abur-Rabiy´ – yaani ´Amr bin Sulaymaan – ametuhadithia: Abul-Ashhab amenihadithia, kutoka kwa Muhammad bin Waasiy´, ambaye amesema:

”Luqmaan alimwambia mwanawe: ”Ee mwanangu kipenzi! Usijifunze usiyoyajua mpaka uyatendee kazi kwanza yale ambayo tayari umeshajifunza.”

86 – Abul-Hasan Muhammad bin ´Abdil-´Aziyz bin Ja´far al-Bardha´iy ametukhabarisha: ´Aliy bin Muhammad bin Ibraahiym bin ´Alluuyah al-Jawhariy ametukhabarisha: Muhammad bin Ahmad bin al-Hasan bin Baabuuyah al-Hinnaa-iy ametuhadithia: ´Abdullaah bin Muhammad al-Qurashiy ametuhadithia: Muhammad bin al-Husayn al-Burjaaniy ametuhadithia: Ahmad bin Muhammad amenihadithia: Abu ´Abdis-Swamad al-´Ammiy amenihadithia, kutoka kwa Maalik bin Diynaar, aliyesema:

”Nimesoma katika baadhi ya hekima: ”Hakuna kheri yoyote kwako kwa wewe kujua kitu ulichokuwa hukijui kisha usikitendee kazi. Kwani mtu kama huyo ni kama mchuma kuni ambaye anafunga matita ya kuni na akashindwa kuyabeba, kisha akafunga matita ya kuni mengine.”

87 – Ahmad bin Ja´far al-Qatwiy´iy ametukhabarisha: Ishaaq bin Sa´d bin al-Hasan bin Sufyaan an-Nasawiy ametukhabarisha: Babu yangu ametuhadithia: Harmalah bin Yahyaa ametuhadithia: Ibn Wahb ametukhabarisha: Sufyaan ametuhadithia:

”Katika wana wa israaiyl alikuwepo mwanachuoni na mfanya ´ibaadah. Yule mwanachuoni akamwambia yule mfanya ´ibaadah: ”Ni kipi kinachokuzuia kuja na kusoma kwangu ilihali unawaona wengine wote wananijia?” Yule mfanya ´ibaadah akajibu: ”Nimejifunza kitu ninachofikiria kukifanyia kazi. Nitapokimaliza, nitakujilia.”

  • Mhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin ´Aliy al-Khatwiyb al-Baghdaadiy (afk. 463)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Iqtidhwaa’-ul-´Ilm al-´Amal, uk. 55-57
  • Imechapishwa: 12/05/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy