84 – Sa´d bin Abiy Waqqaas (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema: “Mwenye kusema wakati atakapomsikia muadhini:

أَشْهَدُ أَنْ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَحْدَهُ لاَ شَرِيكَ لَهُ وَأَنَّ مُحَمَّداً عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ، رَضِيتُ بِاللَّهِ رَبَّاً، وَبِمُحَمَّدٍ رَسُولاً، وَبِالْإِسْلاَمِ دِينَاً

“Nashuhudia ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah, hali ya kuwa yupekee hana mshirika, na kwamba Muhammad ni mja na Mtume Wake. Nimeridhia Allaah kuwa Mola, Muhammad kuwa Mtume na Uislamu kuwa ndio dini yangu.”

atamsamehe dhambi zake.”

Ibn Rumh amesema katika upokezi wake:

“Mwenye kusema wakati atakapomsikia muadhini:

وَأَنَا أَشْهَدُ

“Nami nashuhudia…. “[1]

Ameipokea Muslim.

MAELEZO

Ataisema du´aa hii baada ya shahaadah mbili baada ya kumuitikia muadhini. Baada ya hapo ndio atasema:

وَأَنَا أَشْهَدُ أَنْ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَحْدَهُ لاَ شَرِيكَ لَهُ وَأَنَّ مُحَمَّداً عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ، رَضِيتُ بِاللَّهِ رَبَّاً، وَبِمُحَمَّدٍ رَسُولاً، وَبِالْإِسْلاَمِ دِينَاً

“Na mimi nashuhudia ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah, hali ya kuwa yupekee hana mshirika, na kwamba Muhammad ni mja na Mtume Wake. Nimeridhia Allaah kuwa Mola, Muhammad kuwa Mtume na Uislamu kuwa ndio dini yangu.”

au atasema:

أَشْهَدُ أَنْ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَحْدَهُ لاَ شَرِيكَ لَهُ وَأَنَّ مُحَمَّداً عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ، رَضِيتُ بِاللَّهِ رَبَّاً، وَبِمُحَمَّدٍ رَسُولاً، وَبِالْإِسْلاَمِ دِينَاً

“Nashuhudia ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah, hali ya kuwa yupekee hana mshirika, na kwamba Muhammad ni mja na Mtume Wake. Nimeridhia Allaah kuwa Mola, Muhammad kuwa Mtume na Uislamu kuwa ndio dini yangu.”

Hayo atayasema kabla ya maneno yake muadhini kusema:

حي على الصلاة

“Njooni katika swalah.”

Si kama wanavyodhania baadhi ya watu kwamba yatasemwa mwishoni mwa adhaana.

[1] Muslim (386).

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 88
  • Imechapishwa: 27/10/2025