83 – Abu Sa´iyd al-Khudriy (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Mtaposikia wito basi semeni kama anavosema muadhini.”[1]
Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.
MAELEZO
Ndani yake kuna uwekwaji Shari´ah wa kumuitikia muadhini kwa mwenye kusikia wito ya kwamba aseme kama anavosema muadhini isipokuwa atapofika katika:
حي على الصلاة
حي على الفلاح
Hapo atasema:
لا حَوْلَ وَلَا قُوَّةَ إِلَّا بِاللَّهِ
“Hapana uwezo wa kutikisika wala nguvu isipokuwa kwa msaada wa Allaah.”
Kwa sababu maana yake ni kwamba njooni na harakieni swalah. Ni wito wa kuja kuswali. Kwa vile mtu hawezi jambo hilo isipokuwa kwa msaada wa Allaah ndipo ikasuniwa kusema:

Bi maana sina uwezo wa kutoka katika hali moja kwenda katika hali nyingine nikaweza kuitikia wito na kumuitikia muadhini isipokuwa kwa msaada na nguvu Zako, ee Allaah.
[1] al-Bukhaariy (661) na Muslim (383).
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 87
- Imechapishwa: 26/10/2025
83 – Abu Sa´iyd al-Khudriy (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Mtaposikia wito basi semeni kama anavosema muadhini.”[1]
Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.
MAELEZO
Ndani yake kuna uwekwaji Shari´ah wa kumuitikia muadhini kwa mwenye kusikia wito ya kwamba aseme kama anavosema muadhini isipokuwa atapofika katika:
حي على الصلاة
حي على الفلاح
Hapo atasema:
لا حَوْلَ وَلَا قُوَّةَ إِلَّا بِاللَّهِ
“Hapana uwezo wa kutikisika wala nguvu isipokuwa kwa msaada wa Allaah.”
Kwa sababu maana yake ni kwamba njooni na harakieni swalah. Ni wito wa kuja kuswali. Kwa vile mtu hawezi jambo hilo isipokuwa kwa msaada wa Allaah ndipo ikasuniwa kusema:
لا حَوْلَ وَلَا قُوَّةَ إِلَّا بِاللَّهِ
“Hapana uwezo wa kutikisika wala nguvu isipokuwa kwa msaada wa Allaah.”
Bi maana sina uwezo wa kutoka katika hali moja kwenda katika hali nyingine nikaweza kuitikia wito na kumuitikia muadhini isipokuwa kwa msaada na nguvu Zako, ee Allaah.
[1] al-Bukhaariy (661) na Muslim (383).
Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 87
Imechapishwa: 26/10/2025
https://firqatunnajia.com/19-duaa-wakati-wa-kumsikia-muadhini/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket