18. Du´aa wakati wa kuingia na wakati wa kutoka msikitini

82 – Abu Humayd, au Abu Usayd, amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

اللَّهُمَّ افْتَحْ لي أبْوابَ رَحْمَتِكَ

“Ee Allaah! Nifungulie milango ya rehema Zako.”

Na akitoka aseme:

اللَّهُمَّ إنِّي أسْأَلُكَ مِن فَضْلِكَ

“Ee Allaah! Hakika mimi nakuomba kutokana na fadhilah Zako.”[1]

MAELEZO

Katika Hadiyth hii kuna uwekwaji Shari´ah wa kusema Dhikr hii wakati wa kuingia msikitini na wakati wa kutoka msikitini. Hekima ya kusema Dhikr hii wakati wa kuingia na wakati wa kutoka msikitini: ni kwamba wakati wa kuingia msikitini anakuwa mwenye kuelekea kutekeleza ´ibaadah hii na kwa ajili hiyo ndio maana anamuomba Allaah kutokana na rehema Zake, na wakati wa kutoka anamuomba Allaah kutokana na fadhilah na riziki Zake.

[1] Muslim (713).

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 86
  • Imechapishwa: 27/10/2025