81 – Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) kwa mnasaba wa kulala kwake nyumbani kwa mama yake mdogo Maymuunah, akataja Hadiyth kuhusu Tahajjud yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kisha akasema: “Akaadhini mwadhini kwa ajili ya Subh, akatoka kwa ajili ya kwenda kuswali na huku akisema:
اللَّهُمَّ اجْعَلْ فِي قَلْبِي نُوراً، وفي لِسانِي نُوراً، وَاجْعَلْ فِي سَمْعِي نُوراً ، وَاجْعَلْ فِي بَصَرِي نُوراً، وَاجْعَلْ مِنْ خَلْفِي نُوراً، وَمِنْ أمامي نُوراً ، وَاجْعَلْ مِنْ فَوْقِي نُوراً، وَمِنْ تَحْتِي نُوراً ، اللَّهُمَّ أعْطِني نُوراً
“Ee Allaah! Weka ndani ya moyo wangu nuru, katika ulimi wangu nuru, weka usikizi wangu nuru, weka uoni wangu nuru, weka nyumani kwangu nuru, mbele yangu nuru na chini yangu nuru. Ee Allaah! Nipe nuru.”[1]
Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.
Imekuja katika tamko la Muslim:
وَعَنْ يَمِينِي نُورًا ، وَعَنْ يَسَارِي نُورًا
”… kuliani kwangu nuru, kushotoni kwangu nuru.”
Pia imekuja:
وَعَظُمْ لِي نُورًا
”… nifanyie kubwa nuru yangu,
Pia imekuja:
وَاجْعَلْ لِي نُورًا
”… nifanyie mimi nuru.”
MAELEZO
Haya ni maneno ambayo Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ameyahifadhi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ndani yake kuna du´aa hii tukufu. Kunaombwa du´aa ya nuru. Kinachokusudiwa ni nuru ya elimu, ya imani na ya yakini. Yule ambaye atatiwa nuru moyoni mwake basi moyo wake unakuwa na uhai, anakuwa mwepesi wa utiifu na kuuelekea. Aidha anajiepusha na maasi. Hili ni kwa mujibu wa nguvu na udhaifu wa nuru hiyo. Watu wanatofautiana juu yake kiasi kikubwa. Du´aa hii imewekwa katika Shari´ah kuisoma ndani ya swalah na wakati anapokuwa njiani kuelekea msikitini.
[1] al-Bukhaariy (6316) na Muslim (763).
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 85
- Imechapishwa: 27/10/2025

Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 85
Imechapishwa: 27/10/2025
https://firqatunnajia.com/17-duaa-ya-kwenda-msikitini/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket