19. Watoto chini ya miaka 7 msikitini wanaoshawishi waswaliji

Swali 19: Kuna watoto wenye umri kati ya miaka minne au mitano ambao wanakuja pamoja na wazazi wao kwa ajili ya kuswali ijumaa. Wakati imamu anaposwali wanazikata swalah za waswaliji, wanazungumza na wanatoka nje. Je, haya ni sahihi[1]?

Jibu: Ni lazima kwa wazazi wasiwalete watoto wao wadogo walio chini ya miaka saba mpaka wawe na akili. Wanapofikisha miaka saba na wanaelewa mambo hapo imesuniwa kuwaamrisha swalah. Lakini wakiwa chini ya hivo au hawana akili basi haitakikani kuwaleta. Kwa sababu hawana swalah. Jengine wanawadhuru waswaliji na kuwashawishi.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (12/408-409).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam Swalaat-il-Jumu´ah wal-Jamaa´ah, uk. 59
  • Imechapishwa: 28/11/2021