Miongoni mwa adabu zake zilizo thabiti na zinazotiliwa maanani ni kwamba ailinde mikono yake wakati wa kusomesha dhidi ya mchezo, macho yake dhidi ya kutawanya mtazamo bila haja, akae akiwa na twahara hali ya kuelekea Qiblah, akae kwa heshima na mavazi yake yawe meupe na safi. Anapofika mahali pa kukaa, basi aswali Rak´ah mbili kabla ya kukaa, ni mamoja mahali hapo iwe ni msikiti au si msikiti. Ikiwa ni msikiti, basi hilo ni lenye kusisitizwa zaidi, kwani inachukizwa kukaa humo kabla ya kuswali Rak´ah mbili. Akae kwa kujikunja miguu akitaka au kwa mtindo mwingine. Abu Bakr bin Abiy Daawuud as-Sijistaaniy ameipokea kwa cheni ya wapokezi Swahiyh:
”´Abdullaah bin Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) alikuwa akiwafundisha watu katika msikiti akiwa hali ya kuwa amepiga magoti yake.”
- Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Tibyaan fiy Aadaabi Hamalat-il-Qur-aan, uk. 32
- Imechapishwa: 26/08/2026
Miongoni mwa adabu zake zilizo thabiti na zinazotiliwa maanani ni kwamba ailinde mikono yake wakati wa kusomesha dhidi ya mchezo, macho yake dhidi ya kutawanya mtazamo bila haja, akae akiwa na twahara hali ya kuelekea Qiblah, akae kwa heshima na mavazi yake yawe meupe na safi. Anapofika mahali pa kukaa, basi aswali Rak´ah mbili kabla ya kukaa, ni mamoja mahali hapo iwe ni msikiti au si msikiti. Ikiwa ni msikiti, basi hilo ni lenye kusisitizwa zaidi, kwani inachukizwa kukaa humo kabla ya kuswali Rak´ah mbili. Akae kwa kujikunja miguu akitaka au kwa mtindo mwingine. Abu Bakr bin Abiy Daawuud as-Sijistaaniy ameipokea kwa cheni ya wapokezi Swahiyh:
”´Abdullaah bin Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) alikuwa akiwafundisha watu katika msikiti akiwa hali ya kuwa amepiga magoti yake.”
Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Tibyaan fiy Aadaabi Hamalat-il-Qur-aan, uk. 32
Imechapishwa: 26/08/2026
https://firqatunnajia.com/19-mkao-wa-mwalimu/