Miongoni mwa adabu zake zilizo thabiti na zinazopaswa kulindwa ni kwamba asiidhalilishe elimu kwa namna ya kwenda kwenye mahali panapohusishwa na anayejifunza kutoka kwake ili amfundishe mahali hapo. Haijalishi hata kama mwanafunzi ni khaliyfah au aliye chini yake. Bali aihifadhi elimu kutokana na hilo kama walivyoihifadhi Salaf (Radhiya Allaahu ´anhum). Masimulizi yao katika hili ni nyingi na yanayotambulika.

  • Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tibyaan fiy Aadaabi Hamalat-il-Qur-aan, uk. 33
  • Imechapishwa: 26/08/2026