19. Mitihani inayompata muumini isiyoisha

86 – ´Abdul-A´laa ametuhadithia, kutoka kwa Ma´mar, kutoka kwa az-Zuhriy, kutoka kwa Sa´iyd bin al-Musayyab, kutoka kwa Abu Hurayrah, aliyesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allâhu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mfano wa muumini ni kama mmea; upepo hauachi kuuinamisha kama ambavo mitihani haiachi kumpata muumini. Kafiri ni kama mfano wa mti mwerezi usiotikisika mpaka uvunwe.”[1]

87 – Ibn Numayr ametuhadithia: Zakariyyaa ametueleza, kutoka kwa Sa´d bin Ibraahiym: Ibn Ka´b bin Maalik amenihadithia, kutoka kwa baba yake Ka´b, aliyeeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mfano wa muumini ni kama bua laini ambao unainamishwa na upepo; mara unaukunja, mara unauweka sawa, mpaka unarekebika. Mfano wa kafiri ni kama mti mwerezi imara; hakuna kinachoinama mpaka ung´olewe mara moja.”[2]

88 – Wakiy´ ametuhadithia, kutoka kwa ´Imraan bin Hudayr, kutoka kwa Yahyaa bin Sa´iyd, kutoka kwa Bashiyr bin Nahiyk, kutoka kwa Abu Hurayrah, ambaye amesema:

“Mfano wa muumini dhaifu ni kama bua laini, ambao unainamishwa na upepo na wakati mwingine unaurekebisha.” Nikasema: “Ee Abush-Sha´thaa´[3], vipi kuhusu muumini mwenye nguvu?” Akasema: “Ni kama mtende; kila mwaka unaleta mazao kwenye kivuli chake na wala hauinamishwi na upeo.”[4]

89 – Ghundur ametuhadithia, kutoka kwa Shu´bah, kutoka kwa Ya´laa bin ´Atwaa’, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa ´Abdullaah bin ´Amr, ambaye amesema:

“Mfano wa muumini ni kama mtende; hulisha wema na unaacha vilivyo vizuri.”[5]

[1] Cheni ya wapokezi ni Swahiyh kwa mujibu wa sharti za al-Bukhaariy na Muslim. Muslim ameipokea kupitia cheni ya wapokezi ya mtunzi wa kitabu. at-Tirmidhiy ameipokea kupitia kwa ´Abdur-Razzaaq, kutoka kwa Ma´mar, na ameisahihisha.

[2] Cheni ya wapokezi ni Swahiyh kwa mujibu wa sharti za al-Bukhaariy na Muslim. Muslim ameipokea kupitia cheni ya wapokezi ya mtunzi wa kitabu. Ameipokea tena al-Bukhaariy kwa Sufyaan, kutoka kwa Sa´d bin Ibraahiym, ambaye Ibn Ka´b amemwita ´Abdullaah. Katika upokezi mwingine wa Muslim amemwita kama ´Abdur-Rahmaan. al-Bukhaariy ameipokea tena kwa cheni ya wapokezi pungufu kupitia kwa Zakariyyaa.

[3] Hii ni kun-ya ya Bashiyr bin Nahiyk. Haikutajwa katika “al-Muswannaf”.

[4] Cheni ya wapokezi ni Swahiyh.

[5] Watu watatu wameipokea pia kupitia kwa Shu´bah, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Vilevile imepokelewa kupitia njia nyingine, kutoka kwa Ibn ´Amr, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Nimezihakiki zote katika “as-Swahiyhah” (350).

  • Mhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiy Shaybah al-Kuufiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-Iymaan, uk. 36-37
  • Imechapishwa: 13/07/2023
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy