Swali: Sisi tuko na maeneo ya Shaykh ndani ya msikiti tangu hapo zamani. Baadhi ya watu wakasema tupabomoe na wengine wakasema tupaache. Ni kipi unachotunasihi?

Jibu: Ikiwa maeneo hayo wajinga wanatafuta baraka kwapo, wanaona kuwa yanawaponya wagonjwa wao, wanapapasa udongo wake wanaochukua na mfano wa hayo, basi kutapobomolewa kwa sababu ni katika misingi ya shirki.

Lakini maeneo hayo yakiwa ni chumba au sehemu nyingine ya kufundisha Qur-aan au kufundisha elimu, basi hapana neno muda wa kuwa hakuna mambo yanayopelekea katika shirki; hapapaswi, hauchukuliwi udongo wake wala hakuchupwi mpaka kwa Shaykh kwa kumwomba badala ya Allaah. Si venginevyo mahali hapo kumejengwa ili kufundisha elimu au kusoma mahali hapo Qur-aan na hakuna mambo yanayopelekea katika shirki na wala hakuna mambo yanayopelekea kuchupa mpaka kwa Shaykh, basi katika hali hiyo hapana neno.

Mara nyingi maeneo hayo – kama khabari zilivyotufikia – ni kwamba hakusalimiki na jambo la kupetuka mpaka na kwamba wajinga kupalenga kutafuta baraka, kupapasa, kumwomba Shaykh mahali hapo na mfano wa mambo kama hayo. Haya ni maovu na hayajuzu. Kunapokuwa kunafanywa mambo hayo maeneo hayo basi italazimika kuyaondosha kama ambavo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alivyoondosha al-´Uzzaa, al-Laat, Manaat na maeneo na mizimu mingine ya washirikina kwa lengo la kuziba milango ya shirki na kutokomeza sababu za mtihani.

Ikiwa maeneo hayo lipo kaburi basi hili ni baya zaidi na zaidi. Ikiwa kuna kaburi basi ni lazima kuliondosha nje ya msikiti na ni lazima kulichimbua na kulipeleka katika makaburi ya waislamu na mahala pale kufanywe msikiti ili waislamu waswalie mahali hapo. Kaburi lichimbuliwe na kuondoshwa ikiwa liko ndani ya msikiti. Lakini ikiwa msikiti umejengwa juu yake kwa sababu ya kaburi hilo, basi msikiti ndio utapobomolewa na kuondoshwa na mahali hapo yatakuwa ni  maeneo ya makaburi ambapo watu watazikwa. Msikiti utaondolewa na kutajengwa msikiti mahali kwengine juu ya watu waliohai sehemu ambayo hakuna makaburi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tahdhiyr min Fitnat-il-Qubuur, uk. 78-79
  • Imechapishwa: 05/05/2022