19. Je, inafaa kwa mwanamke kupangusa juu ya mtandio wake?

Swali 19: Je, inafaa kwa mwanamke kupangusa juu ya mtandio wake?

Jibu: Maoni yaliyotangaa kwa Hanaabilah ni kwamba inajuzu ikiwa umezungushwa shingoni mwake. Hili limepokelewa kutoka kwa baadhi ya wakeze Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum).

Ikiwa kuna uzito wa kuvua mtandio kwa sababu ya baridi au kuna uzito kwa mtu kuuvua kisha akauvaa tena, ni sawa kupangusa juu yake. Vinginevyo bora ni kutokufanya hivo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Buhuuth wa Fataawaa fiyl-Mas´h ´alaal-Khuffayn, katika Majmuu´-ul-Fataawaa (11/171)
  • Imechapishwa: 06/05/2021