19. Hadiyth “Hufuta madhambi ya mwaka uliopita na mwaka ujao”

Abu Qataadah al-Answaariy (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliulizwa kuhusu kufunga siku ya ´Arafah ambapo akajibu:

“Hufuta madhambi ya mwaka uliopita na mwaka ujao.”[1]

Ameipokea Muslim.

Hadiyth hii ni dalili ya fadhilah ya kufunga siku ya ´Arafah na thawabu kubwa mbele ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala), kwa sababu kufunga siku hiyo kunafuta madhambi ya miaka miwili. Kufunga siku ya ´Arafah kunapendekezwa kwa wakazi walioko majumbani. Kuhusu mahujaji haipendekezwi kufunga siku hiyo. Badala yake napendekezwa afungue akifuata mfano wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa hivyo inampasa muislamu ambaye ni mkazi afanye pupa ya kufunga siku hii tukufu ili kupata thawabu.

[1] Muslim (1162).

  • Muhusika: Shaykh ´Abdullaah bin Swaalih al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahaadiyth ´Ashrah Dhil-Hijjah wa Ayaam-it-Tashriyq, uk. 33
  • Imechapishwa: 13/05/2025