101 – Baadhi ya wanazuoni – mmoja wao ni Ahmad bin Hanbal (Radhiya Allaahu ´anh) – wamesema kwamba Jahmiy ni kafiri na sio katika waislamu. Damu yake ni halali kumwagwa. Hafai kurithi wala kurithiwa, kwa sababu wanakanusha swalah ya ijumaa, swalah ya mkusanyiko, swalah mbili za ´iyd wala zakaah. Aidha wamesema kwamba yule ambaye hasemi kuwa Qur-aan ni kiumbe ni kafiri. Wakahalalisha upanga dhidi ya ummah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wakaenda kinyume na waliokuwa kabla yao. Wakawapa watu mtihani kwa kitu ambacho hakikuzungumzwa na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wala yeyote katika Maswahabah zake. Wakataka kuitokomeza misikiti na sehemu za kuswalia. Wakaudhoofisha Uislamu. Wakaitokomeza Jihaad na wakatenda kwa ajili ya mfarakano. Wakaenda kinyume na masimulizi na wakazungumza kwa yaliyofutwa. Wakatumia hoja kwa Aayah zisizokuwa wazi na hapo ndipo wakawafanya watu kutilia shaka ´Aqiydah na dini yao. Wakagawanyika juu ya Mola Wao, wakapinga adhabu ndani ya kaburi, Hodhi, Uombezi na wakaona kuwa Pepo na Moto bado havijaumbwa.
Wakapinga mengi katika yaliyosemwa na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ndipo wakahalalisha waliyohalalisha kuwakufurisha na damu zao kwa mtazamo huu. Yule mwenye kukanusha Aayah katika Kitabu cha Allaah, basi amekanusha Kitabu chote, na yule mwenye kukanusha moja katika masimulizi yake Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), basi amekanusha masimulizi yote na hivyo ni mwenye kumkufuru Allaah Mtukufu.
Kukapita kwao muda fulani. Wakapata msaada wa mfalme katika hilo na wakauweka upanga na bakora chini ya hilo. Elimu ya Sunnah na Mkusanyiko ikachakaa na wakazidhoofisha. Zote mbili zikawa ni zenye kufichikana kwa sababu ya kudhiri kwa Bid´ah na falsafa na kwa sababu ya wingi wao. Wakashika utawala vikao vya elimu, wakadhihirisha maoni yao na wakaandika vitabu juu yavyo. Wakawapendekeza watu na wakawatafutia uongozi. Ikawa ni mtihani mkubwa kwelikweli. Hakuna aliyesalimika nao isipokuwa yule aliyekingwa na Allaah. Jambo dogo ambalo mtu alikuwa anaweza kukumbana nalo katika vikao vyao vya elimu, ni kuanza kuishuku dini yake, kuwafuata au kudai kuwa wako katika haki, na wakati huohuo yeye hajui kuwa yuko katika haki au batili. Matokeo yake anakuwa ni mwenye mashaka. Watu wakaangamia mpaka yalipofika masiku ya Ja´far – ambaye pia anaitwa al-Mutawakkil. Allaah akamfanya akaweza kuizima Bid´ah na kuidhihirisha haki. Kupitia kwake Ahl-us-Sunnah wakaweza kudhihiri na maneno yao yakaenea pamoja na kuwa walikuwa wachache na Ahl-ul-Bid´ah ndio walikuwa wengi. Hali iko hivyo mpaka hii leo. Michoro na alama za upotevu bado vimebaki na kuna watu wanayatendea kazi na kulingania kwavyo. Hakuna anayewakataza na hakuna mwenye kuwazuia kwa yale wanayoyasema na kuyafanya!
- Mhusika: Imaam Abu Muhammad al-Hasan bin Khalaf al-Barbahaariy (kfk. 329)
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh-us-Sunnah, uk. 100-102
- Imechapishwa: 22/12/2024

Mhusika: Imaam Abu Muhammad al-Hasan bin Khalaf al-Barbahaariy (kfk. 329)
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh-us-Sunnah, uk. 100-102
Imechapishwa: 22/12/2024
https://firqatunnajia.com/19-ahl-us-sunnah-ni-wachache-mpaka-hii-leo/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)