Swali 18: Je, ni ipi hukumu ya kuondosha Shari´ah ya Kiislamu na kuibadilisha kwa sheria zilizotungwa na wanadamu kama kanuni za kifaransa, za kingereza na nyinginezo, huku ikifanywa kuwa kanuni inayotamka kwamba masuala ya ndoa na mirathi yatatekelezwa kwa mujibu wa Shari´ah ya Kiislamu?
Jibu: Hili ni jambo ambalo wanazuoni wamelizungumzia kwa upana. Haafidhw Ibn Kathiyr (Rahimahu Allaah) ametaja kwamba yeyote anayebadilisha Shari´ah ya Kiislamu kwa nyinginezo za kibinadamu, basi hili ni aina ya ukafiri. Alitoa mfano wa wamongolia waliovamia nchi za Kiislamu na kuweka kanuni za mchanganyiko wa vyanzo mbalimbali walivyoita (الياسق) na akabainisha ukafiri wao. Hili pia limetajwa na Shaykh Muhammad bin Ibraahiym Aalish-Shaykh (Rahimahu Allaah) ambaye alisema katika mwanzo wa kitabu ”Tahkiym-ul-Qawaaniyn”:
“Hakika miongoni mwa ukafiri wa wazi ni kubadilisha Shari´ah iliyo wazi kwa sheria zilizotungwa za laana.”
Kwa hiyo iwapo mtu atabadilisha Shari´ah yote ya Kiislamu kanuni zilizotungwa na wanadamu kutoka mwanzo hadi mwisho, basi hili ni aina ya ukafiri na kuritadi.
Wanazuoni wengine, akiwemo Shaykh ´Abdul-Aziyz bin Baaz (Rahimahu Allaah), wameeleza kwamba ni lazima kiongozi huyo aone kuwa alivofanya inafaa na kwamba ni lazima asimamishiwe hoja, kwa sababu anaweza kuwa ni mjinga wa jambo hilo na hana elimu yoyote. Kwa hiyo ni lazima abainishiwe mpaka hoja isimamishwe juu yake. Akishasimamishiwa hoja, basi hapo ndipo anaweza kuhukumiwa ukafiri. Ni muhimu kuelewa kuwa suala hili ni nyeti sana na ni khatari, khaswa ikiwa mtu aliyepitisha kanuni hizo hana matendo mengine ya kikafiri. Hata hivyo ikiwa mtu huyo tayari ameshafanya aina nyingine za ukafiri, basi hakuna shaka katika hukumu ya ukafiri wake.
Ikiwa tutazingatia mtu ambaye hana matendo mengine ya kikafiri isipokuwa kubadilisha Shari´ah ya Kiislamu, basi wanazuoni wanatofautiana: Je, kitendo cha kubadilisha dini peke yake kinatosha kuwa ukafiri mkubwa, kama alivyosema Haafidhw Ibn Kathiyr na Shaykh Muhammad bin Ibraahiym (Rahimahumaa Allaah), au ni lazima kumsimamishia hoja na kubainisha ya kwamba kitendo hicho ni ukafiri? Hoja ikishambainikia ndipo atahukumiwa ukafiri.
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: As-ilah wa Ajwibah fiy-Iymaan wal-Kufr, uk. 45-46
- Imechapishwa: 07/01/2026

Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: As-ilah wa Ajwibah fiy-Iymaan wal-Kufr, uk. 45-46
Imechapishwa: 07/01/2026
https://firqatunnajia.com/18-ni-ipi-hukumu-ya-kuondosha-shariah-ya-kiislamu-na-kuibadilisha-kwa-sheria-zilizotungwa-za-kizungu/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket