Imaam Abu Bakr Muhammad bin Ishaaq bin Khuzaymah amesema katika kitabu  chake ”Kitaab-ut-Tawhiyd”, ambacho nimekisikia kutoka kwa mjukuu wake Abu Twaahir (Rahimahu Allaah):

”Mlango: Kuthibitisha khabari zilizothibiti na zilizosihi, ambazo wanazuoni wa Hijaaz na ´Iraaq wamezipokea kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusu kushuka kwa Mola (´Azza wa Jall) katika mbingu ya chini –  pasi na kuifanyia namna sifa ya Ushukaji, lakini kwa kuithibitisha.

Tunashuhudia ushuhuda wa kuthibitisha kwa ndimi zetu na kusadikisha kwa mioyo yetu na kuyakinisha yale yaliyotajwa katika khabari hizi ambazo zimetaja kushuka kwa Mola. Hata hivyo hatuifanyii namna, kwa sababu Mtume wetu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakutueleza namna ya anavyoshuka Mola wetu katika mbingu ya dunia. Licha ya hivyo wanazuoni wametufunza kuwa Anashuka. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amembebesha jukumu Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) la kuwabainishia waislamu yale wanayoyahitaji katika mambo ya dini yao. Kwa hivyo sisi tunazithibitisha khabari hizo zinazohusiana na Ushukaji pasi na kupekua namna ya ushukaji, kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakutueleza namna ya Ushukaji.”[1]

Haafidhw Abu ´Abdillaah al-Haakim ametukhabarisha: Abu Muhammad as-Swaydalaaniy ametuhadithia: ´Aliy bin al-Husayn bin al-Junayd ametuhadithia: Ahmad bin Swaalih al-Miswriy ametuhadithia: Ibn Wahb ametuhadithia: Makhramah bin Bukayr ametukhabarisha, kutoka kwa baba yake…

al-Haakim vilevile ametukhabarisha: Muhammad bin Ya´quub al-Aswamm ametuhadithia – na tamko ni lake yeye – Ibraahiym bin Munqidh ametuhadithia: Ibn Wahb ametuhadithia, kutoka kwa Makhramah bin Bukayr, kutoka kwa baba yake: Nimemsikia Muhammad bin al-Mundakar akisema kuwa amemsikia Umm Salamah, mkewe Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), akisema:

”Ni uzuri wa siku iliyoje ambapo Allaah (Ta´ala) anashuka katika mbingu ya chini!” Kukasemwa: ”Ni siku gani hiyo?” Akasema: ”Siku ya ´Arafah.”

[1] Kitaab-ut-Tawhiyd (1/289-290).

  • Mhusika: Imaam Abu ´Uthmaan Ismaa´iyl bin ´Abdir-Rahmaan as-Swaabuuniy (afk. 449)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Aqiydat-us-Salaf wa Aswhaab-il-Hadiyth, uk. 223-226
  • Imechapishwa: 10/12/2023