3- Kula au kunywa kwa makusudi. Amesema (Ta´ala):
وَكُلُوا وَاشْرَبُوا حَتَّىٰ يَتَبَيَّنَ لَكُمُ الْخَيْطُ الْأَبْيَضُ مِنَ الْخَيْطِ الْأَسْوَدِ مِنَ الْفَجْرِ ۖ ثُمَّ أَتِمُّوا الصِّيَامَ إِلَى اللَّيْلِ
“Kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu uzi mweupe wa alfajiri kutokana na uzi mweusi Kisha timizeni funga mpaka usiku.”[1]
Kula na kunywa kwa kusahau ni jambo lisiloathiri funga yake. Imepokelewa katika Hadiyth:
“Ambaye atakula au akanywa kwa kusahau, basi akamilishe funga yake. Kwani si venginevyo Allaah ndiye kamlisha na kumnywesha.”[2]
Miongoni mwa mambo yanayomfunguza mfungaji ni kufikisha maji na mfano wake tumboni kupitia puani. Nacho ni kile kinachoitwa “ugoro”. Vilevile kuingiza virutubisho kwa njia ya mishipa na kumwingiza damu mfungaji. Yote hayo yanaharibu swawm yake kwa sababu ni kumpa chakula.
Miongoni mwa mambo hayo vilevile ni kumdunga mfungaji sindano za lishe. Sindano hizo zinashika nafasi ya chakula, kitu ambacho kinaharibu funga yake. Kuhusu sindano za kawaida mfungaji anatakiwa kuziepuka kwa ajili ya kuilinda swawm yake. Vilevile amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Acha kile chenye kukutia mashaka na kiendee kile kisichokutia mashaka.”[3]
Acheleweshe kufanya hivo mpaka wakati wa usiku.
[1] 02:187
[2] al-Bukhaaariy (6669) na Muslim (2709).
[3] Ahmad (1723), at-Tirmidhiy (2523), an-Nasaa´iy (5727) na al-Haakim (2216). at-Tirmidhiy amesema:
“Hadiyth hii ni nzuri na Swahiyh.”
- Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Mulakhasw al-Fiqh (01/383)
- Imechapishwa: 24/04/2021

Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Mulakhasw al-Fiqh (01/383)
Imechapishwa: 24/04/2021
https://firqatunnajia.com/18-kifunguzi-cha-tatu-cha-funga/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)