2- Kutokwa na manii kwa sababu ya kubusu, kugusa, punyeto au kutazamatazama. Kukipatikana kitu katika hayo basi funga yake inaharibika. Vilevile atalazimika kulipa siku hiyo pasi na kuhitajia kutoa kafara. Kwani kutoa kafara ni jambo maalum wakati wa kufanya jimaa.

Mwenye kulala akiota akatokwa na manii basi hakuna kinachomlazimu. Funga yake ni sahihi. Kwa sababu imetokea pasi na kutaka kwake. Lakini hata hivyo atalazimika kuoga kutokana na janaba.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Mulakhasw al-Fiqh (01/382)
  • Imechapishwa: 04/04/2021