6 – Muwaalaah [kiungo kimoja kisiwahi kukauka kabla ya kuoshwa cha kufuatia]. Ni kwamba mtu afuatanishe kuosha viungo vya wudhuu´ bila kuvikatisha. Kwa maana nyingine ni kwamba asioshe kiungo kimoja kisha akashughulika kwa muda kabla ya kuendelea na kingine, isipokuwa tu ikiwa kuchelewa kwake ni kwa sababu ndogo kama kufungua mlango ulio karibu, basi hilo halidhuru. Dalili ya uwajibu wa jambo hilo ni Hadiyth ya ´Umar bin al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ´anh) kwamba:
“Mtu mmoja alitawadha kisha akaacha sehemu ya kucha katika mguu wake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamwona na akasema: ”Rudi ukafanye vizuri wudhuu´ wako” ambapo akarudi kisha akaswali.”
Ameipokea Muslim (243).
Hadiyth nyingine ya mtu mmoja miongoni mwa Maswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba:
“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimuona mtu akiswali na katika kisigino cha mguu wake kulikuwa na doa dogo la kiasi cha dirhamu halikufikiwa na maji, basi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamuamrisha arudie wudhuu´ na swalah.”
Ameipokea Abu Daawud (175). Tazama ”Irwaa’-ul-Ghaliyl” (86).
Njia ya kujengea dalili kutoka katika Hadiyth hizi mbili juu ya ulazima wa Muwaalaah ni kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakumuamuru yule aliyemuona sehemu ya mguu wake haikufikiwa na maji kwamba aioshe tu sehemu hiyo pekee, bali alimuamuru arudie wudhuu´ wote. Na lau kama Muwaalaah ingekuwa si lazima, ingelitosha tu kwamba aoshe sehemu hiyo ambayo haikufikiwa na maji.
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 19
- Imechapishwa: 21/05/2026
6 – Muwaalaah [kiungo kimoja kisiwahi kukauka kabla ya kuoshwa cha kufuatia]. Ni kwamba mtu afuatanishe kuosha viungo vya wudhuu´ bila kuvikatisha. Kwa maana nyingine ni kwamba asioshe kiungo kimoja kisha akashughulika kwa muda kabla ya kuendelea na kingine, isipokuwa tu ikiwa kuchelewa kwake ni kwa sababu ndogo kama kufungua mlango ulio karibu, basi hilo halidhuru. Dalili ya uwajibu wa jambo hilo ni Hadiyth ya ´Umar bin al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ´anh) kwamba:
“Mtu mmoja alitawadha kisha akaacha sehemu ya kucha katika mguu wake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamwona na akasema: ”Rudi ukafanye vizuri wudhuu´ wako” ambapo akarudi kisha akaswali.”
Ameipokea Muslim (243).
Hadiyth nyingine ya mtu mmoja miongoni mwa Maswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba:
“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimuona mtu akiswali na katika kisigino cha mguu wake kulikuwa na doa dogo la kiasi cha dirhamu halikufikiwa na maji, basi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamuamrisha arudie wudhuu´ na swalah.”
Ameipokea Abu Daawud (175). Tazama ”Irwaa’-ul-Ghaliyl” (86).
Njia ya kujengea dalili kutoka katika Hadiyth hizi mbili juu ya ulazima wa Muwaalaah ni kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakumuamuru yule aliyemuona sehemu ya mguu wake haikufikiwa na maji kwamba aioshe tu sehemu hiyo pekee, bali alimuamuru arudie wudhuu´ wote. Na lau kama Muwaalaah ingekuwa si lazima, ingelitosha tu kwamba aoshe sehemu hiyo ambayo haikufikiwa na maji.
Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 19
Imechapishwa: 21/05/2026
https://firqatunnajia.com/18-faradhi-ya-sita-ya-wudhuu/