Imaam Abu ´Abdillaah ´Amr bin ´Uthmaan al-Makkiy (Rahimahu Allaah) amesema, baada ya kutaja maneno marefu katika msingi wa Tawhiyd:
“Basi Yeye (Ta´ala) ndiye aliyesema:
إِنِّي أَنَا اللَّـهُ رَبُّ الْعَالَمِينَ
”Hakika Mimi ni Allaah, Mola wa walimwengu!”[1]
Siyo mti uliyesema hivo. Yeye ndiye mwenye kuja kabla ya kuja. Siyo mti Yake iliyokuja. Yeye ndiye amelingana juu ya ´Arshi Yake kwa utukufu wa Ukuu Wake, bila ya kuwa mahali popote. Ndiye aliyemzungumzisha Muusa kwa mazungumzo ya kweli na akamwonyesha baadhi ya alama Zake tukufu. Basi Muusa akasikia maneno ya Allaah, mrithi wa viumbe Wake, mwenye kusikia sauti zao, mwenye kuyaangalia kwa jicho Lake maumbo yao. Mikono Yake miwili imekunjuliwa, na hiyo siyo neema Yake wala uwezo Wake. Amemuumba Aadam kwa mkono Wake” na akataja mambo mengine.”
Imaam Abu Bakr Ahmad bin ´Amr bin Abiy ´Aaswim an-Nabiyl amesema:
“Kila kilichomo katika kitabu chetu ”Kitaab-us-Sunnah al-Kabyir” ambacho kina milango ya khabari tulizozitaja kuwa zinapelekea elimu, basi sisi tunaziamini kutokana na kusihi kwake na na uadilifu wa wapokezi wake. Ni lazima kujisalimisha nazo juu ya dhahiri yake na kuacha kupekua namna yake.”[2]
Basi akataja kushuka Kwake hadi mbingu ya chini na kulingana Kwake juu ya ´Arshi.
Zakariyyaa bin Yahyaa as-Saajiy, ambaye ni mwalimu wa al-Ash´ariy, amesema katika Fiqh na Hadiyth:
“´Aqiydah ambayo niliwaona juu yake maswahibu wetu Ahl-ul-Hadiyth ni kuwa Allaah (Ta´ala) yuko juu ya ´Arshi Yake juu ya mbingu Yake. Anakaribia viumbe Wake jinsi atakavyo… ”
Imaam Abu Ja´far Muhammad bin Jariyr at-Twabariy amesema:
”Inamtosha mtu ajue kuwa Mola wake ndiye ambaye amelingana juu ya ´Arshi. Basi yeyote anayepita mipaka zaidi ya hapo, hakika huyo amepata khasara na amefilisika.”[3]
Imaam Abuu Ja´far Ahmad bin Muhammad bin Salaamah at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) katika ´Aqiydah yake mashuhuri:
Huu ni ubainifu wa ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah kwa mujibu wa madhehebu ya wanachuoni wa Uislamu Abu Haniyfah an-Nu´maan bin Thaabit al-Kuufiy, Abu Yuusuf bin Ibraahiym al-Answaariy na Abu ´Abdillaah Muhammad bin al-Hasan ash-Shaybaaniy na yale wanayoamini katika misingi ya dini na kumuabudu kwayo Mola wa walimwengu – Allaah awawie radhi.
1 – Tunasema kuhusu upwekekaji wa Allaah hali ya kuwa ni wenye kuitakidi kwa tawfiyq ya Allaah ya kwamba Allaah ni mmoja asiyekuwa na mshirika. Hakuna kitu mfano Wake. Hakuna chenye kumshinda. Hapana mungu wa haki asiyekuwa Yeye. Qur-aan ni maneno ya Allaah. Kwake ndio imeanza kwa njia ya maneno, jambo ambalo halitakiwi kufanyiwa namna, na Akaiteremsha kwa Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa njia ya Wahy. Kwa haki kabisa waumini wamesadikisha jambo hilo na kuyakinisha kuwa ni maneno ya Allaah (Ta´ala) kikweli. Hayakuumbwa kama maneno ya viumbe. Yule mwenye kuyasikia na akadai kuwa ni maneno ya mtu basi amekufuru… Kuonekana ni haki kwa watu wataokuwa Peponi – pasi na kumzunguka wala kulifanyia namna… Tafsiri yake ni kama alivokusudia Allaah (Ta´ala) na kujua. Hadiyth zote Swahiyh zilizopokelewa kuhusu hilo kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mambo ni kama alivosema… Hakuna ambaye mguu wake utakuwa imara katika Uislamu isipokuwa kwa kujisalimisha. Yule mwenye kujipinda kuyajua yale asiyokuwa na elimu nayo na asikinaike na kujisalimisha, basi atakosa Tawhiyd takasifu, maarifa ya kweli na imani sahihi… Yule asiyeacha ukanushaji na ufananishaji, atapotea na wala hatopatia matakaso yoyote… ´Arshi na Kursiy ni haki. Hata hivyo haihitajii ´Arshi na vyenginevyo. Amekizunguka kila kitu na Yeye yuko juu yake. Amewafanya viumbe Wake wasiweze kuyazunguka.”[4]
[1] 28:30
[2] as-Sunnah (1/215).
[3] Swariyh-us-Sunnah, uk. 27.
[4] al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 2-6.
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Ahmad bin ´Abdil-Haadiy al-Maqdisiy (afk. 744)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Kalaam ´alaa Mas-alat-il-Istiwaa’ ´alaal-´Arsh, uk. 69-71
- Imechapishwa: 23/12/2025

Muhusika: Imaam Muhammad bin Ahmad bin ´Abdil-Haadiy al-Maqdisiy (afk. 744)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Kalaam ´alaa Mas-alat-il-Istiwaa’ ´alaal-´Arsh, uk. 69-71
Imechapishwa: 23/12/2025
https://firqatunnajia.com/18-amepata-khasara-na-amefilisika/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket