Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) amesema kuwa jihaad imepita katika hatua mbalimbali:
1 – Wakati ambapo ilikuwa imekatazwa. Kipindi hichi ni pale ambapo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na waislamu walikuwa Makkah. Walikuwa wameamrishwa kuizuia mikono yao, kusimamisha swalah na kutoa zakaah:
أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ قِيلَ لَهُمْ كُفُّوا أَيْدِيَكُمْ وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ
“Je, huoni wale walioambiwa zuieni mikono yenu na simamisheni swalah na toeni zakaah.”[1]
Wamekatazwa kwa sababu kipindi hicho waislamu walikuwa hawawezi na walikuwa hawana dola wala nguvu. Allaah alikuwa akimwamrisha Mtume Wake kustahamili, kupuuzilia mbali na kusubiri mpaka pale kutapokuja faraja. Anayepigana katika kipindi hicho alikuwa amemuasi Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa sababu kipindi hicho kupigana kulikuwa kunaweza kupelekea waislamu wakadhurika na ulinganizi. Matokeo yake makafiri wakawatawala waislamu.
2 – Pindi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipohamia Madiynah na ikasimama dola ya Kiislamu. Hapo ndipo walipewa idhini ya kupigana vita pasi na kuamrishwa:
أُذِنَ لِلَّذِينَ يُقَاتَلُونَ بِأَنَّهُمْ ظُلِمُوا ۚ وَإِنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ نَصْرِهِمْ لَقَدِيرٌ الَّذِينَ أُخْرِجُوا مِن دِيَارِهِم بِغَيْرِ حَقٍّ إِلَّا أَن يَقُولُوا رَبُّنَا اللَّـهُ ۗ وَلَوْلَا دَفْعُ اللَّـهِ النَّاسَ بَعْضَهُم بِبَعْضٍ لَّهُدِّمَتْ صَوَامِعُ وَبِيَعٌ وَصَلَوَاتٌ وَمَسَاجِدُ يُذْكَرُ فِيهَا اسْمُ اللَّـهِ كَثِيرًا
“Wameruhusiwa kupigana wale wanaopigwa kwa kuwa wamedhulumiwa na hakika Allaah bila shaka ni Muweza wa kuwanusuru; ambao wametolewa majumbani mwao bila ya haki isipokuwa kwa kuwa tu wanasema: “Mola wetu ni Allaah na lau ingelikuwa Allaah hawakingi watu baadhi yao kwa wengine, basi bila shaka yangelivunjwa mahekalu na makanisa na masinagogi na misikiti inayotajwa humo jina la Allaah kwa wingi.”[2]
Hapo ndipo walipewa ruhusa bila kuamrishwa. Hiyo ilikuwa hali ya kuwaandaa. Mambo magumu Allaah anayawekea Shari´ah kidogo kidogo kwa ajili ya kuwasahilishia watu.
3 – Wakati ambapo waliamrishwa kuwapiga vita wenye kuwapiga vita na kujizuia kutokamana na wasiowapiga vita:
وَقَاتِلُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ الَّذِينَ يُقَاتِلُونَكُمْ وَلَا تَعْتَدُوا ۚ إِنَّ اللَّـهَ لَا يُحِبُّ الْمُعْتَدِينَ
“Piganeni katika njia ya Allaah na wale ambao wanakupigeni wala msichupe mipaka. Hakika Allaah hawapendi wenye kuchupa mipaka.”[3]
Hii inaitwa jihaad ya kujitetea.
4 – Pindi waislamu walipokuwa na nguvu na Uislamu ukawa na dola wakaamrishwa kupigana vita kwa hali zote:
فَإِذَا انسَلَخَ الْأَشْهُرُ الْحُرُمُ فَاقْتُلُوا الْمُشْرِكِينَ حَيْثُ وَجَدتُّمُوهُمْ وَخُذُوهُمْ وَاحْصُرُوهُمْ وَاقْعُدُوا لَهُمْ كُلَّ مَرْصَدٍ
“Itapomalizika miezi mitukufu, basi waueni washirikina popote muwakutapo, wafanyeni mateka na wahusuruni na wakalieni katika kila sehemu ya uvamizi. Lakini wakitubu na wakasimamisha swalah na wakatoa zakaah, basi waacheni huru.”[4]
وَقَاتِلُوهُمْ حَتَّى لاَ تَكُونَ فِتْنَةٌ وَيَكُونَ الدِّينُ لِلّهِ
“Piganeni nao mpaka kusiweko shirki na dini yote iwe kwa ajili ya Allaah pekee.”[5]
Allaah akaamrisha kupambana vita kwa hali zote. Walipokuwa wameshajiandaa na tayari wako na nguvu na maandalizi, ndipo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akaweka Shari´ah ya vita; vita vya Badr, vita vya Uhud, Khandaq na vyenginevyo. Hali iliendelea hivo mpaka kulipokuja Ufunguzi na watu wakaingia katika dini ya Allaah makundi kwa makundi.
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akafa na kukatokea kuritadi ambapo Abu Bakr akapambana nao. Alipomaliza kuwashughulikia akaanza kupambana na makafiri na kutayarisha majeshi kuwapiga vita wafursi na warumi. Alipokufa akaja ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) na yeye akaendelea na kazi ya Ufunguzi mpaka akaangusha dola ya Kisraa na Qayswar. Dini ikaenea na ikatawala ulimwenguni kote mashariki na magharibi. Haya ndio mapambano katika Uislamu.
[1] 04:77
[2] 22:39-40
[3] 02:190
[4] 09:05
[5] 08:39
- Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 189-190
- Imechapishwa: 08/12/2024

Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 189-190
Imechapishwa: 08/12/2024
https://firqatunnajia.com/174-hatu-za-jihaad/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)