Ni lazima kwa waislamu wahiji kila mwaka. Kuhusu mtu mmoja mmoja akihiji mtu mara moja inatosha. Atakayezidisha itakuwa ni jambo linalopendeza.

Ni nani anayesimamisha hajj? Kiongozi wa waislamu ndiye anayetakiwa kuwaongoza mahujaji, kutangaza siku ya ´Arafah, kusimama nao siku ya ´Arafah, kwenda Muzdalifah na pia kumfuata katika nembo zilizosalia – ni mamoja kiongozi mwenyewe ndiye anahiji nao au mwakilishi wake. Jambo lisiwe la vurugu. Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wanahiji pamoja na viongozi wao. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kufunga kunakuwa siku ile wamefunga wengine, na Adhwhaa inakuwa siku ile wamechinja wengine.”[1]

Namna hiyo ndio unakuwa ummah wa kiislamu. Wanafunga pamoja pale ambapo inaafikiana miandamo yao, wanahiji kwa pamoja, wanaswali ´iyd kwa pamoja. Mkusanyiko ni miongoni mwa alama za Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah, na mipasuko ni miongoni mwa alama za Ahl-ul-Bid´ah na wapotofu.

[1] at-Tirmidhiy (696), Abu Daawuud (2324), na Ibn Maajah (1660). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh-ul-Jaamiy´” (4287).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 187
  • Imechapishwa: 08/12/2024