Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

135 – Kuhiji na kupigana jihaad ni mambo yenye kuendelea na mtawala wa kiislamu, ni mamoja mwema na muovu wao, mpaka kisimame Qiyaamah. Hakuna kitu kitakachoyabatilisha wala kuyaondoa.

MAELEZO

Tumeshatangulia kutaja suala la kuswali nyuma ya viongozi, ni mamoja ni wema au watenda madhambi. Tunaswali nyuma yao kwa ajili ya kutekeleza amri ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa sababu ametuamrisha kuwatii na akatukataza kuwaasi. Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) walitekeleza amri yake na wakawa wanaswali nyuma ya viongozi hata kama wanafanya baadhi ya madhambi makubwa. Kufanya hivo ni kwa ajili ya kuleta umoja. Hii ndio ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah tofauti na wanavoona Khawaarij na Mu´tazilah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 186
  • Imechapishwa: 08/12/2024