69 – Abul-Hasan ´Aliy bin Ahmad bin ´Umar al-Muqriy ametukhabarisha: ´Abdul-Baaqiy bin Qaaniy´ al-Qaadhwiy ametuzindua: al-Husayn bin ´Aliy bin al-Azhar ametuhadithia huko Kuufah: ´Abbaad bin Ya´quub ametuhadithia: Abu Daawuud an-Nakha´iy ametuhadithia: ´Aliy bin ´Ubaydillaah al-Ghatwafaaniy ametuhadithia, kutoka kwa Sulayk: Nimemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:
”Mwanachuoni anayewafunza watu kheri na akajisahau mwenyewe ni kama mfano wa taa linalowaangazia watu na kujichoma yenyewe.”[1]
70 – Abu Nu´aym Ahmad bin ´Abdillaah bin Ahmad bin Ishaaq al-Haafidhw ametukhabarisha huko Aswbahaan: Abu Muhammad ´Abdullaah bin Ja´far bin Ahmad bin Faaris ametuhadithia: Ismaa´iyl bin ´Abdillaah bin Mas´uud al-´Abdiy ametuhadithia: Hishaam bin ´Ammaar ametuhadithia: ´Aliy bin Sulaymaan al-Kalbiy ametuhadithia: al-A´mash ametuhadithia, kutoka kwa Abu Tamiymah, kutoka kwa Jundub bin ´Abdillaah, aliyesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Mfano wa mwanachuoni anayewafunza watu kheri na akajisahau mwenyewe ni kama mfano wa taa linalowamulikia watu na kujichoma yenyewe.”[2]
71 – Muhammad bin Ahmad bin Rizq ametukhabarisha: al-Husayn bin Ayyuub al-Haashimiy ametukhabarisha: Muusa bin ´Iysaa al-Misswiyswiy ametuhadithia: Luwayn ametuhadithia… Yuusuf bin Rabaah bin ´Aliy al-Baswriy pia ametukhabarisha: al-Qaadhwiy Abul-Hasan ´Aliy bin al-Husayn bin Bundaar al-Adhaniy ametuzindua: Luwayn ametuhadithia… al-Hasan bin Muhammad al-Khallaal pia amenikhabarisha: Muhammad bin ´Aliy bin Suwayd ametuhadithia: Muhammad bin ´Aliy bin Daawuud at-Tamiymiy ametuzindua huko Adhanah: Luwayn Muhammad bin Sulaymaan ametuhadithia: Muhammad bin Jaabir ametuhadithia, kutoka kwa Yuunus bin ´Ubayd, kutoka kwa al-Hasan, kutoka kwa Abu Barzah, aliyesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Mfano wa mwanachuoni anayewafunza watu kheri na akajisahau mwenyewe ni kama mfano wa utambi unaowamulikia watu na kujichoma wenyewe.”[3]
Tamko ni la al-Khallaal.
72 – al-Hasan bin Abiy Bakr ametukhabarisha: Abul-Husayn ´Abdus-Swamad bin ´Aliy bin Muhammad at-Twastiy ametukhabarisha: Muhammad bin al-Qaasim, anayejulikana pia kama Abul-´Aynaa’, ametuhadithia: Abu ´Aaswim ametuhadithia, kutoka kwa Ibn Jurayj, kutoka kwa Abuz-Zubayr, kutoka kwa Jaabir, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ambaye amesema:
”Kundi la watu wa Peponi watawaona kundi la watu wa Motoni waseme: ”Ni kipi kilichokuingizeni Motoni? Hakika si vyenginevyo kilichotufanya kuingia Peponi ni kwa ajili ya kukufunzeni.” Ndipo waseme: ”Tulikuwa tukikuamrisheni na hatutendi.”[4]
[1] Cheni ya wapokezi imetungwa kwa sababu ya Abu Daawuud Sulaymaan bin ´Amr at-Twaa-iy, ambaye alikuwa akitambulika kwa uwongo.
[2] Hadiyth ni Swahiyh. at-Twabaraaniy ameipokea katika “al-Mu´jam al-Kabiyr” (1/84/2) kupitia njia mbili zingine kutoka kwa Hishaam bin ´Ammaar. Cheni hii ya wapokezi ni nzuri. Wasimulizi wake ni wenye kutambulika isipokuwa tu ´Aliy bin Sulaymaan al-Kalbiy. Ibn Abiy Haatim amesimulia kutoka kwa baba yake alisema juu yake:
”Sioni ubaya wowote juu ya Hadiyth zake. Hadiyth zake ni njema, lakini hatambuliki.” (al-Jarh wat-Ta´diyl (3/1/188-189))
at-Twabaraaniy pia ameisimulia kupitia kwa Layth, kutoka kwa Swafwaan bin Mihraz, kutoka kwa Jundub bin ´Abdillaah. Cheni hii ya wapokezi haina neno kwa lengo la ufuatiliaji. Isitoshe inatiwa nguvu na Hadiyth ya Abu Barzah inayofuatia.
[3] Hadiyth Swahiyh kupitia ilio kabla yake. Humo yumo Muhammad bin Jaabir as-Suhaymiy ambaye alikuwa dhaifu kutokana na kumbukumbu yake mbaya, inasilihi kwa lengo la kutilia nguvu. Kupitia njia yake at-Twabaraaniy ameipokea katika “al-Mu´jam al-Kabiyr” na ad-Daamighaaniy katika “al-Ahaadiyth wal-Akhbaar” (1/110/2).
[4] Cheni yake ya wapokezi ni dhaifu sana. Abul-´Aynaa´ amekiri kutunga na akasema mwenyewe:
”Mimi na al-Jaahidhw tulikuwa tukitunga Hadiyth kuhusu Fadak.”
ad-Daaraqutwniy amesema kuwa ”sio mwenye nguvu katika Hadiyth”. Jengine ni kwamba Ibn Jurayj na Abuz-Zubayr walikuwa wenye hadhaa – na katika Hadiyth hii hakubainisha amesikia simulizi hiyo kutoka kwa nani.
- Muhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin ´Aliy al-Khatwiyb al-Baghdaadiy (afk. 463)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Iqtidhwaa’-ul-´Ilm al-´Amal, uk. 48-50
- Imechapishwa: 12/05/2024
- Taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)