4 – Upokezi wa Ja’far bin Maymuun[1]

Imaam Abu Ismaa´iyl as-Swaabuuniy amesema: Abul-Hasan bin Ishaaq al-Madaniy ametuhadithia: Ahmad bin al-Khadhwir Abul-Hasan ash-Shaafi’iy[2] ametuhadithia: Shaadhaan ametuhadithia: Ibn Makhlad bin Yaziyd al-Qahastwaaniy ametuhadithia: Ja’far bin Maymuun ametuhadithia:

“Maalik bin Anas aliulizwa kuhusu maneno Yake:

الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ

”Mwingi wa rehema amelingana juu ya ´Arshi.”[3]

na namna Alivyolingana. Akajibu: “Kulingana juu si kitu kisichotambulika. Namna haitambuliki. Kuamini hilo ni wajibu na kuuliza juu yake ni Bid´ah. Mimi sikuoni vyengine isipokuwa mpotevu.” Kisha akaamuru afukuzwe kutoka kwenye kikao chake.”

[1] Abu ´Aliy, kwa jina jingine Abul-´Awwaam, Ja’far bin Maymuun at-Tamiymiy al-Anmaatwiy. Amepokea kutok kwa Abul-´Aaliyah na ´Atwaa’ bin Abiy Rabaah na wengineo. Sufyaan ath-Thawriy, Sufyaan bin ´Uyaynah, Yahyaa bin Sa´iyd al-Qatwaan na wengineo wamepokea kutoka kwake. Ahmad amesema hana nguvu katika kusimulia. an-Nasaa’iy amesema mfano wa hayo. Ibn Ma’iyn amesema kuwa hakuwa na nguvu sana. Katika sehemu nyingine amesema kwamba hakuwa mwaminifu. Amesema sehemu nyingine ya tatu kwamba alikuwa salama katika kusimulia. Abu Haatim amesema kuwa alikuwa salama. Labda hii ndiyo sababu ad-Daaraqutwniy  kusema kuwa ni mwenye kuzingatiwa. Tazama “Tahdhiyb-ul-Kamaal” (5/114-115). Ibn Hajar amesema juu yake:

“Mkweli anayekosea.” Alikuwa ni katika watu wa tabaka la sita.” (at-Taqriyb (969))

[2] Ahmad bin al-Khadhwir bin Ahmad bin al-Hasan an-Naysaabuuriy ash-Shaafi´iy. adh-Dhahabiy amesema juu yake:

“Mwenye kuhifadhi, mwenye kusoma Qur-aan vyema,  mwanachuoni wa Fiqh… ni mmoja katika maimamu wakubwa… Alifariki katika Jumaadaa al-Aakhirah mnamo 344.” (Siyar A´laam-in-Nubalaa’ (15/501)

[3] 20:05

  • Muhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Allaamah ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad al-Badr
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Athar al-Mash-huur ´an-il-Imaam Maalik fiy Swifat-il-Istiwaa’, uk. 35-36
  • Imechapishwa: 29/11/2025