313 – ´Aliy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
إسباغُ الوُضوء في المكارهِ، وإعمالُ الأقدامِ إلى المساجِد، وانتظارُ الصلاةِ بعد الصلاةِ؛ تَغسِلُ الخطايا غَسْلاً
“Kueneza vizuri wudhuu´ wakati wa machukizo, hatua nyingi kwenda misikitini na kusubiri swalah nyingine baada ya swalah kumalizika kunaosha makosa kikwelikweli.”[1]
Ameipokea Abu Ya´laa na al-Bazzaar kwa cheni ya wapokezi Swahiyh.
[1] Swahiyh.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/246)
- Imechapishwa: 02/12/2022
- Taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy