17. Hadiyth “Kama mtu atakuwa katika ardhi changaforo… “

249 – Salmaan al-Faarisiy (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kama mtu atakuwa katika ardhi changaforo na ukaingia wakati wa swalah basi na atawadhe, asipopata maji basi afanye Tayammum, akikimu swalah basi huswali pamoja naye Malaika wawili. Na endapo ataadhini na kukimu swalah, basi wataswali nyuma yake askari wa Allaah ambao hawawezi kuonekana na ncha moja hadi nyingine.”[1]

Ameipokea ´Abdur-Razzaaq kupitia kwa Ibn-ut-Taymiy, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Abu ´Uthmaan an-Nahdiy.

[1] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/218-219)
  • Imechapishwa: 02/03/2022
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy