17. Du´aa ya kuomba ulinzi na maana yake

Shaykh-ul-Islaam na Imaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Kisha mtu anasema:

أعوذ بالله من الشيطان الرجيم

A´udhubi Allaahi min ash-Shaytwaan ar-Rajiym.”

“Najilinda kwa Allaah kutokamana na shaytwaan aliyefukuwa mbali.”

Maana ya “A´udhubi Allaahi” yaani ninaomba kinga na msaada Kwako ewe Allaah. Maana ya “min ash-Shaytwaan ar-Rajiym” yaani aliyefukuzwa na kuwekwa mbali na Rahmah za Allaah, kutokana na kunidhuru duniani na Aakhirah.

MAELEZO

Baada ya kusoma du´aa ya kufungulia swalah anatakiwa kujilinda kwa Allaah kutokamana na shaytwaan aliyefukuzwa. Aseme:

أعوذ بالله من الشيطان الرجيم

 “Najilinda kwa Allaah kutokamana na shaytwaan aliyefukuwa mbali.”

Aseme hivo kabla ya kuanza kusoma.

Maana ya “A´udhubi Allaahi” ni kwamba najilinda, nakimbilia na kukuelekea Wewe kutokamana na shaytwaan ambaye ni adui Yako, aliyefukuzwa.

Shaytwaan aliyefukuzwa bi maana ambaye amefukuzwa na kutiwa mbali na rehema za Allaah. Unasema haya ili asikudhuru katika dini wala dunia yako. Hii ndio maana ya du´aa ya kuomba ulinzi; unakimbilia na kuelekea kwa Allaah kutokamana na shaytwaan ambaye ni adui Yako, aliyefukuzwa.

Swali: Ni ipi hukumu ya kukariri du´aa ya kuomba kinga katika Rak´ah ya pili?

Jibu: Sio lazima. Kwa sababu swalah ni kitu kimoja. Lakini mtu akikariri hakuna ubaya.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ash-Sharh al-Mumtaaz, uk. 102
  • Imechapishwa: 03/07/2018