Harb bin Ismaa´iyl al-Kirmaaniy amesema:
“Jahmiyyah. Ni maadui wa Allaah na ndio wale wanaodai kuwa Qur-aan imeumbwa. Wanadai kuwa Allaah (´Azza wa Jall) hakumzungumzisha Muusa (´alayhis-Salaam), kwamba Allaah hazungumzi na wala haongei. Vilevile wanaona kuwa Allaah hatoonekana, kwamba Hana mahali na kwamba Hana ´Ashiy wala Kursiy. Yapo mengine mengi wanayosema ambayo nachukia kuyataja. Ni makafiri, mazanadiki na maadui wa Allaah. Tahadharini nao!”[1]
Muhammad bin Abiy Shaybah amesema:
”Wanasema ya kwamba Jahmiyyah wanasema kuwa hakuna kitu kinachotenganisha baina ya Allaah na viumbe Wake. Wakakanusha ´Arshi na kwamba Allaah yuko juu yake. Wakasema kuwa Allaah yuko kila mahali… ” Wanazuoni wamefasiri:
وَهُوَ مَعَكُمْ
”Naye Yu Pamoja nanyi.”
kwa maana kwa ujuzi Wake. Kisha Hadiyth zikapokewa kwa wingi ya kuwa Allaah aliumba ´Arshi kisha akalingana juu yake kwa dhati Yake. Kwa hiyo Yeye yuko juu ya ´Arshi kwa dhati Yake hali ya kuwa ametengana na viumbe Wake akiwa mbali nao.”[2]
Imaam Abu Muhammad Ibn Qutaybah amesema:
”Sisi tunasema kuhusu maneno Yake Allaah (Ta´ala):
مَا يَكُونُ مِن نَّجْوَىٰ ثَلَاثَةٍ إِلَّا هُوَ رَابِعُهُمْ
“Hauwi mnong’ono wa watatu isipokuwa Yeye ni wa nne wao.”[3]
ya kwamba maana yake Yeye Yuko pamoja nao kwa kujua yale waliyo nayo. Ni kama vile unavyomwambia mtu aliyesafiri kwenda katika mji wa mbali:
“Tahadhari usipunguze juhudi. Hakika mimi nipo pamoja nawe.”
Unamaanisha kuwa unajua uzembeaji wake. Vipi mtu ataweza kusema kuwa Yeye (Subhaanahu wa Ta´ala) yuko kila mahali, hali ya kuwa Yeye anasema:
الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ
”Mwingi wa rehema amelingana juu ya ´Arshi.”[4]
na:
إِلَيْهِ يَصْعَدُ الْكَلِمُ الطَّيِّبُ وَالْعَمَلُ الصَّالِحُ يَرْفَعُهُ
“Kwake pekee linapanda neno zuri na kitendo chema anakiinua juu.”[5]
Vipi kipande Kwake kitu ilihali Yeye yuko pamoja nacho? Vipi Malaika na Roho watapanda Kwake ilihali Yeye yuko pamoja nao? Lau watu hawa wangerudi katika maumbile yao ambayo wameumbwa nayo ya kumjua Muumba, basi wangelijua kuwa Allaah ndiye Aliyepaa juu, ndiye wa juu kabisa na kwamba mikono huinuliwa kwa du´aa Kwake na kwamba mataifa yote wakiwemo waarabu na wasiokuwa waarabu husema kuwa Allaah yuko juu ya mbingu. Hata hivyo maumbile yao yamebadilika.”[6]
Hata ndani ya Injiyl al-Masiyh aliwaambia wanafunzi wake:
“Mkiwasamehe watu, basi Baba yenu aliye juu mbinguni atawasamehe madhambi yenu. Tazameni ndege wa mbinguni, hawapandi wala hawavuni, lakini Baba yenu aliye juu mbinguni huwapa riziki.”[7]
Kuna mifano mingi kama hii katika mada hii.
[1] Kitaab-us-Sunnah, uk. 80-81.
[2] Kitaab-ul-´Arsh, uk. 276-286.
[3] 58:7
[4] 20:5
[5] 35:10
[6] Ta’wiyl Mukhtalaf-il-Hadiyth, uk. 182-183.
[7] Matayo 6:26
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Ahmad bin ´Abdil-Haadiy al-Maqdisiy (afk. 744)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Kalaam ´alaa Mas-alat-il-Istiwaa’ ´alaal-´Arsh, uk. 67-68
- Imechapishwa: 23/12/2025

Muhusika: Imaam Muhammad bin Ahmad bin ´Abdil-Haadiy al-Maqdisiy (afk. 744)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Kalaam ´alaa Mas-alat-il-Istiwaa’ ´alaal-´Arsh, uk. 67-68
Imechapishwa: 23/12/2025
https://firqatunnajia.com/17-aqiydah-ya-maadui/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket