Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:
132 – Tunawapenda watu waadilifu na waaminifu, na tunawachukia watu wa dhuluma na khiyana.
MAELEZO
Mapenzi ni kitendo cha moyo. Kuna sampuli mbili za mapenzi:
1 – Mapenzi ya kimaumbile, kama mtu kuipenda familia yake, mke wake, watoto wake, marafiki zake, kula na kunywa. Mapenzi haya sio ´ibaadah.
2 – Mapenzi ya kidini. Mapenzi haya yamegawanyika sampuli mbili:
1 – Kumpenda Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Hii ni aina kubwa kabisa ya ´ibaadah. Ibn-ul-Qayyim amesema:
Kumwabudu Mwingi wa rehema ndio kilele cha mwisho cha kumpenda
pamoja na kujidhalilisha kwa mfanya ´ibaadah – hizo ni nguzo mbili
Kwazo ndio kunazungukia nyanja ya ´ibaadah
ambayo, hata hivyo, haizunguki hadi nguzo zote mbili ziinuliwe
Kumwabudu Mwingi wa rehema ndio mwisho wa kumpenda. ´Ibaadah zote zinazungukia katika mapenzi. Mapenzi ni aina kubwa ya ´ibaadah. Haijuzu kumpenda yeyote pamoja na Allaah:
وَلَوْ يَرَى الَّذِينَ ظَلَمُوا إِذْ يَرَوْنَ الْعَذَابَ أَنَّ الْقُوَّةَ لِلَّـهِ جَمِيعًا وَأَنَّ اللَّـهَ شَدِيدُ الْعَذَابِ وَالَّذِينَ آمَنُواْ أَشَدُّ حُبًّا لِّلّهِ
“Lakini wale walioamini wana mapenzi zaidi kwa Allaah. Lau wale waliodhulumu wanaijua [adhabu inayowasubiri] watakapoona adhabu [mbele yao siku hiyo] kwamba nguvu zote ni za Allaah na kwamba hakika Allaah ni mkali wa kuadhibu.”
Huku ni kushirikisha katika mapenzi. Kwa ajili hiyo amesema:
وَالَّذِينَ آمَنُوا أَشَدُّ حُبًّا لِّلَّـهِ
“Wale walioamini wana mapenzi zaidi kwa Allaah.”[1]
Waumini hawampendi isipokuwa Allaah. Mapenzi yao kwa Allaah ni makubwa zaidi kushinda mapenzi ya waabudia masanamu kwa masanamu yao. Kwa sababu mapenzi ya kumpenda Allaah hayakatiki duniani wala Aakhirah. Hilo ni tofauti na mapenzi ya wengine juu ya waungu wao yatakatika huko Aakhirah ambapo kutatokea uadui kati ya waungu wao na wale walikuwa wakiwaabudu:
وَإِذَا حُشِرَ النَّاسُ كَانُوا لَهُمْ أَعْدَاءً وَكَانُوا بِعِبَادَتِهِمْ كَافِرِينَ
“Na [Qiyaamah] watakapokusanywa watu [miungu ya uongo] watakuwa maadui wao na watakuwa kwa ‘ibaadah zao ni wenye kuzikanusha.”[2]
وَقَالَ إِنَّمَا اتَّخَذْتُم مِّن دُونِ اللَّـهِ أَوْثَانًا مَّوَدَّةَ بَيْنِكُمْ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۖ ثُمَّ يَوْمَ الْقِيَامَةِ يَكْفُرُ بَعْضُكُم بِبَعْضٍ وَيَلْعَنُ بَعْضُكُم بَعْضًا وَمَأْوَاكُمُ النَّارُ وَمَا لَكُم مِّن نَّاصِرِينَ
“Na akasema: “Hakika hapana venginevyo mmefanya badala ya Allaah masanamu kuwa ni mapenzi makubwa kati yenu katika maisha ya dunia, kisha siku ya Qiyaamah mtakanushana nyinyi kwa nyinyi na mtalaaniana nyinyi kwa nyinyi na makazi yenu ni Moto na hamtokuwa na wenye kunusuru.”[3]
[1] 2:165
[2] 46:6
[3] 29:25
- Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 177-178
- Imechapishwa: 03/12/2024

Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 177-178
Imechapishwa: 03/12/2024
https://firqatunnajia.com/165-mapenzi-ya-kumpenda-allaah/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)