Namna hiyo imekuja katika Aayah Kursiy:
اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ ۚ لَا تَأْخُذُهُ سِنَةٌ وَلَا نَوْمٌ
”Allaah, hapana mungu wa haki mwingine isipokuwa Yeye, aliyehai daima, msimamia kila kitu. Haumchukui usingizi wala kulala.” (02:255)
Amejikanushia kuchukuliwa na usingizi na kulala. Usingizi ni mzito zaidi kuliko kulala. Amejikanushia haya kwa sababu Yeye (Subhaanah) anasifika kuwa na uhai kamili na timilifu. Kwa sababu ulalaji na usingizi ni upungufu katika uhai. Kwa ajili hiyo Allaah akawa n mwenye kutakaswa kutokana na hayo. Yeye ni ambaye yuhai na hafi. Kulala ni aina ya kifo. Hakika Yeye (Subhaanah) yuhai na hafi:
لَّهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ
“Ni Vyake pekee vilivyomo katika mbingu na vilivyomo katika ardhi.”
Bi maana Yeye ndiye mwenye kuvimiliki vyote hivyo.
- Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah, uk. 24
- Imechapishwa: 19/10/2024
Namna hiyo imekuja katika Aayah Kursiy:
اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ ۚ لَا تَأْخُذُهُ سِنَةٌ وَلَا نَوْمٌ
”Allaah, hapana mungu wa haki mwingine isipokuwa Yeye, aliyehai daima, msimamia kila kitu. Haumchukui usingizi wala kulala.” (02:255)
Amejikanushia kuchukuliwa na usingizi na kulala. Usingizi ni mzito zaidi kuliko kulala. Amejikanushia haya kwa sababu Yeye (Subhaanah) anasifika kuwa na uhai kamili na timilifu. Kwa sababu ulalaji na usingizi ni upungufu katika uhai. Kwa ajili hiyo Allaah akawa n mwenye kutakaswa kutokana na hayo. Yeye ni ambaye yuhai na hafi. Kulala ni aina ya kifo. Hakika Yeye (Subhaanah) yuhai na hafi:
لَّهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ
“Ni Vyake pekee vilivyomo katika mbingu na vilivyomo katika ardhi.”
Bi maana Yeye ndiye mwenye kuvimiliki vyote hivyo.
Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah, uk. 24
Imechapishwa: 19/10/2024
https://firqatunnajia.com/16-uhai-wa-allaah-ni-kamili/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)