86 – Tambua ya kwamba swalah za faradhi ni tano. Hakuzidishwi juu yake na wala nyakati zake hazipunguzwi. Safarini kunaswaliwa Rak´ah mbili isipokuwa tu swalah ya Maghrib. Yule mwenye kusema kuwa ni zaidi ya swalah tano, amezua, na mwenye kusema kuwa ni chini ya tano, amezua. Allaah hakubali chochote katika swalah hizo isipokuwa ndani ya wakati wake, isipokuwa endapo mtu atakuwa ni mwenye kusahau, hapo atakuwa ni mwenye kupewa udhuru. Hivyo basi, aiswali pale tu atapokuikumbuka. Kama mtu ni msafiri anaweza kukusanya baina ya swalah mbili akipendelea kufanya hivo.
87 – Zakaah inatolewa juu ya dhahabu, fedha, matunda, nafaka na wanyama wa kufugwa, kutokana na vile alivosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ikiwa ataigawanya mwenyewe inafaa kufanya hivo na akimpa kiongozi inafaa vilevile kufanya hivo.
88 – Tambua ya kwamba kitu cha kwamza katika Uislamu ni kushuhudia ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad ni mja na Mtume Wake.
89 – Yale Allaah aliyosema ni kama alivyosema na hakuna ukinzani katika yale aliyosema. Naye ni kama Alivosema.
90 – Inatakiwa kuamini mambo yote ya Shari´ah.
91 – Tambua ya kwamba biashara inayoendelea katika masoko ya waislamu ni halali muda wa kuwa imejengeka kwa mujibu wa hukumu ya Qur-aan, Uislamu na Sunnah, bila ya kuingiliwa na ubadilishaji, dhuluma, ukandamizaji, khiyana au kwenda kinyume na Qur-aan au kinyume na ujuzi.
- Mhusika: Imaam Abu Muhammad al-Hasan bin Khalaf al-Barbahaariy (kfk. 329)
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh-us-Sunnah, uk. 95-96
- Imechapishwa: 22/12/2024
86 – Tambua ya kwamba swalah za faradhi ni tano. Hakuzidishwi juu yake na wala nyakati zake hazipunguzwi. Safarini kunaswaliwa Rak´ah mbili isipokuwa tu swalah ya Maghrib. Yule mwenye kusema kuwa ni zaidi ya swalah tano, amezua, na mwenye kusema kuwa ni chini ya tano, amezua. Allaah hakubali chochote katika swalah hizo isipokuwa ndani ya wakati wake, isipokuwa endapo mtu atakuwa ni mwenye kusahau, hapo atakuwa ni mwenye kupewa udhuru. Hivyo basi, aiswali pale tu atapokuikumbuka. Kama mtu ni msafiri anaweza kukusanya baina ya swalah mbili akipendelea kufanya hivo.
87 – Zakaah inatolewa juu ya dhahabu, fedha, matunda, nafaka na wanyama wa kufugwa, kutokana na vile alivosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ikiwa ataigawanya mwenyewe inafaa kufanya hivo na akimpa kiongozi inafaa vilevile kufanya hivo.
88 – Tambua ya kwamba kitu cha kwamza katika Uislamu ni kushuhudia ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad ni mja na Mtume Wake.
89 – Yale Allaah aliyosema ni kama alivyosema na hakuna ukinzani katika yale aliyosema. Naye ni kama Alivosema.
90 – Inatakiwa kuamini mambo yote ya Shari´ah.
91 – Tambua ya kwamba biashara inayoendelea katika masoko ya waislamu ni halali muda wa kuwa imejengeka kwa mujibu wa hukumu ya Qur-aan, Uislamu na Sunnah, bila ya kuingiliwa na ubadilishaji, dhuluma, ukandamizaji, khiyana au kwenda kinyume na Qur-aan au kinyume na ujuzi.
Mhusika: Imaam Abu Muhammad al-Hasan bin Khalaf al-Barbahaariy (kfk. 329)
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh-us-Sunnah, uk. 95-96
Imechapishwa: 22/12/2024
https://firqatunnajia.com/16-namna-hii-ndivo-anavoswali-msafiri/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)