16. Mlango kuhusu maneno Yake (Ta´ala) “Mpaka itakapoondolewa fazaiko nyoyoni mwao [baada ya kuzimia]; watasema [wakiulizana]: “Amesema nini Mola wenu?” – waseme: “Ya haki; Naye yujuu, Mkubwa kabisa.”

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

1- Allaah (Ta´ala) amesema:

حَتَّىٰ إِذَا فُزِّعَ عَن قُلُوبِهِمْ قَالُوا مَاذَا قَالَ رَبُّكُمْ ۖ قَالُوا الْحَقَّ ۖ وَهُوَ الْعَلِيُّ الْكَبِيرُ

”Mpaka itakapoondolewa fazaiko nyoyoni mwao [baada ya kuzimia]; watasema [wakiulizana]: “Amesema nini Mola wenu?” – waseme: “Ya haki; Naye yujuu, Mkubwa kabisa.” (Sabaa´ 34:23)

2- Imesihi kupokelewa kupitia Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) kwamba Mtume (Swalla Allaaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah anapotoa amri huko juu ya mbingu Malaika hupiga mbawa zao kwa kuyanyenyekea maneno Yake. Kama vile ni mnyororo juu ya mlima. Huwapita amri hiyo hali wamezimia mpaka inapoondolewa ile fazaiko kwenye nyoyo zao wanasema [wakiulizana]: “Amesema nini Mola wenu?” – waseme: “Ya haki; Naye yujuu, Mkubwa kabisa.” Husikia Neno hilo wale waibao usikizi na hawa waibao usikizi wanakuwa wamepandiana namna hii. Sufyaan bin ´Uyaynah alionyesha kwa kunyanyua mkono wake na kutawanya vidole. Wadukuzi wa usikizi huliagiza neno hili kwa kwa aliye chini yake, kisha huyo mwingine humuagizia aliye chini yake mpaka humfikishia kuhani au mchawi. Wakati mwingine humpata kimondo kabla ya kuifikisha na wakati mwingine huenda akaifikisha kabla ya kimondo hicho kumpata. Hapo ndipo huongezewa neno hilo uongo mia moja. Kunasemwa: “Kwani sialitwambia hivi na hivi siku kadhaa na kadhaa?” Husadikishwa kwa neno hilo alilolisikia kutoka mbinguni.”[1]

3- an-Nawwaas bin Sam´aan (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah (Ta´ala) anapotaka kufunua amri ya jambo fulani basi Huzungumza. Hapo ndipo mbingu hutetemeka sana – au alisema radi kali – kwa sababu ya kumuogopa Allaah (´Azza wa Jall). Wanapoyasikia hayo wakazi wa mbinguni basi huanguka chini hali ya kusujudu. Wa kwanza wao ambaye hunyanyua kichwa chao anakuwa ni Jibriyl ambaye Allaah anamzungumzisha kwa Wahy kwa Ayatakayo. Kisha Jibriyl anawapitia Malaika wengine katika mbingu mbalimbali. Katika kila tabaka anayopita basi Malaika humuuliza: “Kasema nini Mola Wetu, ee Jibriyl?” Jibriyl anasema: [wakiulizana]: “Amesema nini Mola wenu?” – waseme: “Ya haki; Naye yujuu, mkubwa.” Jibriyl hujibu: “Ya haki; Naye yujuu, Mkubwa kabisa.” Baada ya hapo wote husema vile alivyosema Jibriyl. Jibriyl humalizia kwa Wahy vile Alivyoamrishwa na Allaah (´Azza wa Jall).”[2]

MAELEZO

1- Allaah (Ta´ala) amesema:

حَتَّىٰ إِذَا فُزِّعَ عَن قُلُوبِهِمْ قَالُوا مَاذَا قَالَ رَبُّكُمْ ۖ قَالُوا الْحَقَّ ۖ وَهُوَ الْعَلِيُّ الْكَبِيرُ

”Mpaka itakapoondolewa fazaiko nyoyoni mwao [baada ya kuzimia]; watasema [wakiulizana]: “Amesema nini Mola wenu?” – waseme: “Ya haki; Naye yujuu, Mkubwa kabisa.”

Alichokusudia mtunzi wa kitabu kwa mlango huu ni kuwaraddi waabudu makaburi, masanamu, Malaika na wengineo. Anabainisha namna Malaika wanavyomuogopa Allaah na adhabu Yake pindi ikiwa watakwenda kinyume na amri Yake. Ni vipi basi watashahiki kuabudiwa?

إِنَّ الَّذِينَ تَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ عِبَادٌ أَمْثَالُكُمْ

“Hakika wale muowaombao badala ya Allaah ni waja kama nyinyi.” (al-A´raaf 07:194)

2- Imesihi kupokelewa kupitia Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) kwamba Mtume (Swalla Allaaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah anapotoa amri huko juu ya mbingu Malaika hupiga mbawa zao kwa kunyenyekevu maneno Yake. Kama vile ni mnyororo juu ya mlima. Huwapita amri hiyo hali wamezimia mpaka inapoondolewa ile fazaiko kwenye nyoyo zao wanasema [wakiulizana]: “Amesema nini Mola wenu?” – waseme: “Ya haki; Naye yujuu, Mkubwa kabisa.” Husikia Neno hilo wale waibao usikizi na hawa waibao usikizi wanakuwa wamepandiana namna hii. Sufyaan bin ´Uyaynah alionyesha kwa kunyanyua mkono wake na kutawanya vidole. Wadukuzi wa usikizi huliagiza neno hili kwa kwa aliye chini yake, kisha huyo mwingine humuagizia aliye chini yake mpaka humfikishia kuhani au mchawi. Wakati mwingine humpata kimondo kabla ya kuifikisha na wakati mwingine huenda akaifikisha kabla ya kimondo hicho kumpata. Hapo ndipo huongezewa neno hilo uongo mia moja. Kunasemwa: “Kwani sialitwambia hivi na hivi siku kadhaa na kadhaa?” Husadikishwa kwa neno hilo alilolisikia kutoka mbinguni.”

Mtume (Swalla Allaaahu ´alayhi wa sallam) ametaja fazaiko na namna inavyowaondoka Malaika, kama ilivyokuja katika Hadiyth. Wanapopata fahamu husema: “Amesema nini Mola wenu?” Waseme hali ya kujibu: “Ya haki.” Bi maana wanaambizana. Ya haki kinachokusudiwa ni yale aliyosema Allaah kuhusu hili na lile.

Wakati Malaika wanaposikia neno la Mola (´Azza wa Jall) basi huanza hupiga mbawa zao huku wakiogopa na wakinyenyekea mbele ya Allaah (´Azza wa Jall). Kama kwamba ni minyororo iliyopigwa juu ya mlima. Hapo ndipo wadukuzi wa usikizi huiba maneno haya yaliyosemwa na Malaika. Wanakuwa wamepandiana na baadhi huwaagizia wengine neno hilo mpaka wa mwisho kumfikia huwa ni kuhani au mchawi. Hupatwa na kimondo. Wakati fulani kuna ambao hupatwa na kimondo kabla ya kulifikisha neno lile kwa mchawi na wakati mwingien kuna ambao hulifikisha baada ya kuwa wameshalifikisha. Hivi ndivyo Allaah anawapa mtihani waja Wake. Lau Allaah angetaka basi wasingelisikia chochote. Maneno haya yanamfikia mchawi na anayachanganya na uongo mia moja na ilihali ukweli ni mmoja tu. Ndipo watu wanaanza kuambizana namna kuna siku aliyosema kweli. Matokeo yake wanasadikisha maneno mengi kwa sababu ya neno moja tu la kweli. Kwa ajili hiyo ndio maana haitakiwi kwa mtu akadanganyika na watu hawa. Haitakiwi kuwaamini kunatokamana ima na jambo la kidunia lililonukuliwa kutoka kwa mashaytwaan au kutoka kwa wadukuzi wa usikizi. Kwa hivyo ni wajibu kutowasikiliza japokuwa watakuwa ni wenye kusema kweli wakati fulani.

3- an-Nawwaas bin Sam´aan (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah (Ta´ala) anapotaka kufunua amri ya jambo fulani basi Huzungumza. Hapo ndipo mbingu hutetemeka sana – au alisema radi kali – kwa sababu ya kumuogopa Allaah (´Azza wa Jall). Wanapoyasikia hayo wakazi wa mbinguni basi huanguka chini hali ya kusujudu. Wa kwanza wao ambaye hunyanyua kichwa chao anakuwa ni Jibriyl ambaye Allaah anamzungumzisha kwa Wahy kwa Ayatakayo. Kisha Jibriyl anawapitia Malaika wengine katika mbingu mbalimbali. Katika kila tabaka anayopita basi Malaika humuuliza: “Kasema nini Mola Wetu, ee Jibriyl?” Jibriyl anasema: [wakiulizana]: “Amesema nini Mola wenu?” – waseme: “Ya haki; Naye yujuu, mkubwa.” Jibriyl hujibu: “Ya haki; Naye yujuu, Mkubwa kabisa.” Baada ya hapo wote husema vile alivyosema Jibriyl. Jibriyl humalizia kwa Wahy vile Alivyoamrishwa na Allaah (´Azza wa Jall).”

Sam´aan inaweza pia kusomwa Sim´aan.

Jibriyl pia inaweza kusomwa kama Jabraaiyl. Yeye ndiye wa kwanza anayepata fahamu kwa sababu yeye ndiye Malaika mtukufu zaidi na ndiye mjumbe kati ya Allaah na Mitume Wake. Kila anapopita katika mbingu basi humuuliza Malaika wa mbingu hiyo. Wadukuzi wa usikizi husikia maneno wanayoambizana Malaika. Wakati mwingine huenda wakahifadhi kitu na wakawafikishia wachawi na makuhani. Wakati mwingine huenda wakachomwa na wasifikishe kitu. Allaah ndiye mwamuzi.

Ni wajibu kumuabudu Allaah peke yake. Si Malaika, Mitume wala mwengineo hawaistahiki. Hapa kuna dalili ya kuogopa kwa Malaika na kufazaika kwao.

Yule mwenye kuamini kuwa makuhani wanajua mambo yaliyofichikana ni kafiri.

Katika Hadiyth kuna kuthibiti kwa sifa ya Allaah kuwa na maneno na utashi na fadhilah za Malaika.

Hadiyth inathibitisha vilevile kwamba mashaytwaan hudukua usikizi. Hali ilikuwa hivo hata kabla ya utume. Wakati alipotumilizwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndipo wakawekewa mkazo. Wakati (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipokufa wakawa ni wenye kuendelea kusikiliza. Wakati fulani wanapatwa na kimondo kabla ya kuwahi kusikiliza na wakati mwingine wanapatwa na kimondo baada ya kuwahi kusikiliza.

[1] al-Bukhaariy (7481).

[2] at-Twabaraaniy katika ”Musnad-ush-Shaamiyyiyn” (591).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kitaab-it-Tawhiyd, uk. 60-62
  • Imechapishwa: 03/10/2018