Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

1- Allaah (Ta´ala) amesema:

وَأَنذِرْ بِهِ الَّذِينَ يَخَافُونَ أَن يُحْشَرُوا إِلَىٰ رَبِّهِمْ ۙ لَيْسَ لَهُم مِّن دُونِهِ وَلِيٌّ وَلَا شَفِيعٌ لَّعَلَّهُمْ يَتَّقُونَ

”Na waonye kwayo [Qur-aan] wale wanaokhofu ya kwamba watakusanywa kwa Mola wao; hawana badala  Yake mlinzi wala mwombezi ili wapate kumcha.” (al-An´aam 06:51)

2-

قُل لِّلَّهِ الشَّفَاعَةُ جَمِيعًا

 “Sema: “Uombezi wote ni wa Allaah.” (az-Zumar 39:44)

 3-

مَن ذَا الَّذِي يَشْفَعُ عِندَهُ إِلَّا بِإِذْنِهِ

“Nani huyu ambaye anashufai mbele Yake bila ya idhini Yake?” (al-Baqarah 02:255)

4-

وَكَم مِّن مَّلَكٍ فِي السَّمَاوَاتِ لَا تُغْنِي شَفَاعَتُهُمْ شَيْئًا إِلَّا مِن بَعْدِ أَن يَأْذَنَ اللَّـهُ لِمَن يَشَاءُ وَيَرْضَىٰ

”Na Malaika wangapi mbinguni haitowafaa kitu chochote uombezi wao  isipokuwa baada ya kuwa Allaah ametolea idhini kwa Amtakaye na kumridhia.” (an-Najm 53:26)

5-

قُلِ ادْعُوا الَّذِينَ زَعَمْتُم مِّن دُونِ اللَّهِ لَا يَمْلِكُونَ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ فِي السَّمَاوَاتِ وَلَا فِي الْأَرْضِ وَمَا لَهُمْ فِيهِمَا مِن شِرْكٍ وَمَا لَهُ مِنْهُم مِّن ظَهِيرٍ وَلَا تَنفَعُ الشَّفَاعَةُ عِندَهُ إِلَّا لِمَنْ أَذِنَ لَهُ حَتَّى إِذَا فُزِّعَ عَن قُلُوبِهِمْ قَالُوا مَاذَا قَالَ رَبُّكُمْ قَالُوا الْحَقَّ وَهُوَ الْعَلِيُّ الْكَبِيرُ

”Sema: “Waombeni wale mnadai [kuwa ni waungu] badala ya Allaah. Hawamiliki uzito wa atomu mbinguni wala ardhini na wala wao hawana humo ushirika na wala Hana msaidizi miongoni mwao.” Na wala hautofaa  uombezi mbele Yake isipokuwa kwa yule Aliyempa idhini. Mpaka itakapoondolewa fazaiko nyoyoni mwao [baada ya kuzimia]; watasema [wakiulizana]: “Amesema nini Mola wenu?” – waseme: “Ya haki; Naye yujuu, Mkubwa kabisa.” (Sabaa´ 34:22-23)

6- ´Abul-´Abbaas amesema:

“Allaah amekanusha vyote visivyokuwa Yeye ambavyo washirikina wamejiambatanisha navyo. Amekanusha kwa yeyote badala Yake kuwa na mamlaka au ushirika wowote wa hilo badala Yake au msaidizi wowote kwa Allaah. Hapakubaki isipokuwa uombezi. Hivyo amebainisha ya kwamba hautomfaa yeyote isipokuwa kwa yule ambaye Mola kampa idhini. Kama alivyosema (Ta´ala):

وَلَا يَشْفَعُونَ إِلَّا لِمَنِ ارْتَضَىٰ

“Na wala hawamuombei yeyote yule isipokuwa kwa yule ambaye Amemridhia.” (al-Anbiyaa´ 21:28)

Uombezi huu ambao washirikina wanatumai umekanushwa kuwepo kwake siku ya Qiyaamah, kama ulivyokanushwa na Qur-aan. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameeleza kwamb atakuja na kumsujudia Mola wake na kumhimidi. Hatoanza kuombea moja kwa moja. Baada ya hapo ndipo Ataambiwa:

“Nyanyua kichwa chako. Sema na utasikizwa. Omba na utapewa. Shufai utakubaliwa.[1]

7- Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) alimuuliza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Ni nani katika watu atakayekuwa na furaha zaidi kwa uombezi wako?” Akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Ni yule atakayesema: “Hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah” akiwa ni wenye kutakasika kutoka moyoni mwake.”[2]

Kwa hivyo uombezi huu ni kwa wale wenye Ikhlaasw baada ya idhini ya Allaah. kwa idhini ya Allaah na hautokuwa kwa wale waliomshirikisha Allaah. Ukweli wa mambo ni kwamba Allaah (Subhaanah) ndiye atakayetoa fadhilah Zake kuwapa wale wenye Ikhlaasw na awasamehe kupitia du´aa za waombeaji wataopewa idhini ya kushufai kwa ajili ya kumkirimu na kufikia nafasi yenye kusifiwa. Uombezi ambao umekanushwa na Qur-aan ni ule ambao ndani yake kuna shirki. Kwa ajili hii ndio maana uombezi umethibiti kwa idhini Yake katika maeneo mbalimbali. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amebainisha ya kwamba hautokuwa isipokuwa kwa watu wa Tawhiyd na Ikhlaasw.

MAELEZO

Watu wamezungumzia kuhusu uombezi na wakafikia katika maoni mbalimbali. Wazushi wamepondoka kwa ´Aqiydah zao batili. Kwa ajili hiyo ndio maana wanachuoni wakalazimika kuizungumzia mada hii maalum ili muumini aweze kutambua haki na awe na imani sahihi juu yake. Mlango unaozungumzia uombezi ni wenye kubainisha uombezi uliothibitishwa na uliokanushwa pamoja na haki na batili ndani yake.

 1- Allaah (Ta´ala) amesema:

وَأَنذِرْ بِهِ الَّذِينَ يَخَافُونَ أَن يُحْشَرُوا إِلَىٰ رَبِّهِمْ ۙ لَيْسَ لَهُم مِّن دُونِهِ وَلِيٌّ وَلَا شَفِيعٌ لَّعَلَّهُمْ يَتَّقُونَ

”Na waonye kwayo [Qur-aan] wale wanaokhofu ya kwamba watakusanywa kwa Mola wao; hawana badala  Yake mlinzi wala mwombezi ili wapate kumcha.”

Bi maana, ee Muhammad, waonye kwa Qur-aan wale wanaokhofu kwamba ipo siku watafufuliwa kwa Mola wao. Inawahusu waislamu kwa sababu makafiri hawakusikia na wala hawakuitikia. Maonyo ni matangazo yanayoambatana na makhofisho. Allaah (Ta´ala) amesema:

لَيْسَ لَهُم مِّن دُونِهِ وَلِيٌّ وَلَا شَفِيعٌ لَّعَلَّهُمْ يَتَّقُونَ

“… hawana badala  Yake mlinzi wala mwombezi ili wapate kumcha… “

Huu ni uombezi batili. Waja hawatokuwa na walinzi wala waombezi kabisa isipokuwa wale  atakaowaridhia Allaah. Makafiri wanadhani kuwa watakuwa na walinzi na waombezi ambao watawaokoa kutokamana na Moto kwa sababu walikuwa wakiwaabudu. Kwa sababu hiyo ndio maana walikuwa wakiwaabudu badala ya Allaah:

هَـٰؤُلَاءِ شُفَعَاؤُنَا عِندَ اللَّـهِ

“Hawa ni waombezi wetu mbele ya Allaah.” (Yuunus 10:18)

مَا نَعْبُدُهُمْ إِلَّا لِيُقَرِّبُونَا إِلَى اللَّـهِ زُلْفَىٰ

“Hatuwaabudu isipokuwa ili wapate kutukurubisha kwa Allaah karibu” (az-Zumar 39:03)

Ndipo Allaah akabainisha kuwa watu hawatokuwa na walinzi wala waombezi badala Yake na kwamba uombezi huu wa makafiri ni batili na kwamba uombezi wa haki ni ule ambao Allaah atawaidhinisha Mitume na mawalii kuwaombea wapwekeshaji na waumini na sio makafiri na wanafiki. Allaah (Ta´ala) amesema:

لَّعَلَّهُمْ يَتَّقُونَ

“… ili wapate kumcha.”

Bi maana kwa ajili wamche Allaah na wawe na msimamo juu ya dini Yake pale watapotambua kuwa hakuna uombezi wala mlinzi yeyote badala ya uombezi na ulinzi Wake. Kwa ajili hiyo ndio maana wanatakiwa kumuabudu Yeye pekee na watahadhari kutokamana na ghadhabu Zake.

2-

قُل لِّلَّهِ الشَّفَاعَةُ جَمِيعًا

 “Sema: “Uombezi wote ni wa Allaah.”

Waambie watu kwamba uombezi wote ni wa Allaah. Kabla ya hapo amewakemea wale wenye kudai kuwa na waombezi badala ya Allaah. Wakimaanisha waombezi wao kuwa masanamu, mawe na waungu wao wengine. Allaah akawakanushia hilo:

فَمَا تَنفَعُهُمْ شَفَاعَةُ الشَّافِعِينَ

“Basi haitowafaa uombezi wowote wa waombezi.” (al-Muddaththir 74:48)

وَأَنذِرْ بِهِ الَّذِينَ يَخَافُونَ أَن يُحْشَرُوا إِلَىٰ رَبِّهِمْ ۙ لَيْسَ لَهُم مِّن دُونِهِ وَلِيٌّ وَلَا شَفِيعٌ لَّعَلَّهُمْ يَتَّقُونَ

”Na waonye kwayo [Qur-aan] wale wanaokhofu ya kwamba watakusanywa kwa Mola wao; hawana badala  Yake mlinzi wala mwombezi ili wapate kumcha.”

Uombezi ni Wake pekee. Mitume na waja wema watashufai kwa idhini Yake. Anampa idhini yule Amtakaye. Hivyo ni wajibu kumuomba Yeye na kumuomba ampe idhini Mtume na waja wema wakuombee.

Hakuna ubaya kumuombea uombezi aliyehai wakati wa uhai wake. Mfano wa hilo ni kumuomba mtu mwema akuombee kwa Allaah akusamehe au akuongoze. Ama kuhusu masanamu, wafu, viumbe visivyoonekana, kama mfano wa Malaika, hawatakiwi kuombwa mambo hayo. Kwa sababu hawatambui hali yako. Hawajui mambo yaliyofichikana tofauti na wanavyoamini wajinga na makafiri.

  3-

مَن ذَا الَّذِي يَشْفَعُ عِندَهُ إِلَّا بِإِذْنِهِ

“Nani huyu ambaye anashufai mbele Yake bila ya idhini Yake?”

4-

وَكَم مِّن مَّلَكٍ فِي السَّمَاوَاتِ لَا تُغْنِي شَفَاعَتُهُمْ شَيْئًا إِلَّا مِن بَعْدِ أَن يَأْذَنَ اللَّـهُ لِمَن يَشَاءُ وَيَرْضَىٰ

”Na Malaika wangapi mbinguni haitowafaa kitu chochote uombezi wao  isipokuwa baada ya kuwa Allaah ametolea idhini kwa Amtakaye na kumridhia.”

5-

قُلِ ادْعُوا الَّذِينَ زَعَمْتُم مِّن دُونِ اللَّهِ لَا يَمْلِكُونَ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ فِي السَّمَاوَاتِ وَلَا فِي الْأَرْضِ وَمَا لَهُمْ فِيهِمَا مِن شِرْكٍ وَمَا لَهُ مِنْهُم مِّن ظَهِيرٍ وَلَا تَنفَعُ الشَّفَاعَةُ عِندَهُ إِلَّا لِمَنْ أَذِنَ لَهُ حَتَّى إِذَا فُزِّعَ عَن قُلُوبِهِمْ قَالُوا مَاذَا قَالَ رَبُّكُمْ قَالُوا الْحَقَّ وَهُوَ الْعَلِيُّ الْكَبِيرُ

”Sema: “Waombeni wale mnadai [kuwa ni waungu] badala ya Allaah. Hawamiliki uzito wa atomu mbinguni wala ardhini na wala wao hawana humo ushirika na wala Hana msaidizi miongoni mwao.” Na wala hautofaa  uombezi mbele Yake isipokuwa kwa yule Aliyempa idhini. Mpaka itakapoondolewa fazaiko nyoyoni mwao [baada ya kuzimia]; watasema [wakiulizana]: “Amesema nini Mola wenu?” – waseme: “Ya haki; Naye yujuu, Mkubwa kabisa.” (Sabaa´ 34:23)

Allaah (Subhaanah) amebainisha kwamba hakuna yeyote atakayeombea mbele Yake isipokuwa baada ya idhini Yake na kwamba hatoombewa yeyote isipokuwa kwa  yule Aliyemridhia. Hata Malaika hawamiliki uombezi. Bali ni Allaah pekee ndiye anamiliki. Ikiwa hiyo ndio hali ya Malaika, Manabii na Mitume kwamba hawawezi kushufai isipokuwa baada ya Allaah kuwapa idhini na kumridhia yule mwombewaji, basi waja wema, watoto na wengineo wana haki zaidi ya kutoweza kufanya hivo.

Wale waliofungamana na watu hawa ambao wanawaomba badala ya Allaah wanafungamana nao kwa sababu ya mambo mane ambayo kayabainisha Allaah:

قُلِ ادْعُوا الَّذِينَ زَعَمْتُم مِّن دُونِ اللَّهِ لَا يَمْلِكُونَ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ فِي السَّمَاوَاتِ وَلَا فِي الْأَرْضِ وَمَا لَهُمْ فِيهِمَا مِن شِرْكٍ وَمَا لَهُ مِنْهُم مِّن ظَهِيرٍ وَلَا تَنفَعُ الشَّفَاعَةُ عِندَهُ إِلَّا لِمَنْ أَذِنَ لَهُ حَتَّى إِذَا فُزِّعَ عَن قُلُوبِهِمْ قَالُوا مَاذَا قَالَ رَبُّكُمْ قَالُوا الْحَقَّ وَهُوَ الْعَلِيُّ الْكَبِيرُ

”Sema: “Waombeni wale mnadai [kuwa ni waungu] badala ya Allaah. Hawamiliki uzito wa atomu mbinguni wala ardhini na wala wao hawana humo ushirika na wala Hana msaidizi miongoni mwao.” Na wala hautofaa  uombezi mbele Yake isipokuwa kwa yule Aliyempa idhini. Mpaka itakapoondolewa fazaiko nyoyoni mwao [baada ya kuzimia]; watasema [wakiulizana]: “Amesema nini Mola wenu?” – waseme: “Ya haki; Naye yujuu, Mkubwa kabisa.”

1- Mamlaka. Wanadhani kuwa wanamiliki kitu. Uhakika wa mambo Allaah ndiye ana mamlaka yote.

2- Ushirika. Wanadhani kuwa ni washirika wa Allaah.

3- Msaidizi. Wanadhani kuwa wanamsaidia Allaah, jambo ambalo ni batili.

4- Uombezi. Wanadahni kuwa waungu wao watawaombea.

Allaah akabainisha kwamba hakuna yeyote awezaye kuombea isipokuwa kwa idhini Yake na kwamba hakuna uombezi wenye kujitegemea kama hali ilivyo duniani. Duniani mtu anaweza kukubali uombezi wa mwingine kwa sababu ya kumuogopa na kumuhitajia, mambo ambayo Allaah ametakasika nayo.

6- ´Abul-´Abbaas amesema:

“Allaah amekanusha vyote visivyokuwa Yeye ambavyo washirikina wamejiambatanisha navyo. Amekanusha kwa yeyote badala Yake kuwa na mamlaka au ushirika wowote wa hilo badala Yake au msaidizi wowote kwa Allaah. Hapakubaki isipokuwa uombezi. Hivyo amebainisha ya kwamba hautomfaa yeyote isipokuwa kwa yule ambaye Mola kampa idhini. Kama alivyosema (Ta´ala):

وَلَا يَشْفَعُونَ إِلَّا لِمَنِ ارْتَضَىٰ

“Na wala hawamuombei yeyote yule isipokuwa kwa yule ambaye Amemridhia.” (al-Anbiyaa´ 21:28)

Uombezi huu ambao washirikina wanatumai umekanushwa kuwepo kwake siku ya Qiyaamah, kama ulivyokanushwa na Qur-aan. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameeleza kwamb atakuja na kumsujudia Mola wake na kumhimidi. Hatoanza kuombea moja kwa moja. Baada ya hapo ndipo Ataambiwa:

“Nyanyua kichwa chako. Sema na utasikizwa. Omba na utapewa. Shufai utakubaliwa

Abul-´Abbaas ni Shaykh-ul-Islaam [Ibn Taymiyyah]. Uombezi huu wanaotarajia washirikina siku ya Qiyaamah umekanushwa, kama ilivyotajwa katika Qur-aan. Baadhi yao wanafikiria kwamba masanamu na waungu wao watawaombea kilazima, kwamba hawatohitajia idhini, uombezi wao utakubaliwa, kwamba wataingia Peponi kwa sababu yao na kwamba watasalimishwa kutokamana na Moto. Haya ni kwa haki ya yule ambaye anaamini Aakhirah. Kuhusu yule asiyeamini Aakhirah wanawaomba kwa ajili ya mambo ya kidunia. Malengo yao ya uombezi ni manufaa ya kidunia. Waarabu wengi walikuwa hawaamini Aakhirah.

7- Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) alimuuliza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Ni nani katika watu atakayekuwa na furaha zaidi kwa uombezi wako?” Akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Ni yule atakayesema: “Hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah” akiwa ni wenye kutakasika kutoka moyoni mwake.”

Kwa hivyo uombezi huu ni kwa wale wenye Ikhlaasw baada ya idhini ya Allaah. kwa idhini ya Allaah na hautokuwa kwa wale waliomshirikisha Allaah. Ukweli wa mambo ni kwamba Allaah (Subhaanah) ndiye atakayetoa fadhilah Zake kuwapa wale wenye Ikhlaasw na awasamehe kupitia du´aa za waombeaji wataopewa idhini ya kushufai kwa ajili ya kumkirimu na kufikia cheo chenye kusifiwa. Uombezi ambao umekanushwa na Qur-aan ni ule ambao ndani yake kuna shirki. Kwa ajili hii ndio maana uombezi umethibiti kwa idhini Yake katika maeneo mbalimbali. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amebainisha ya kwamba hautokuwa isipokuwa kwa watu wa Tawhiyd na Ikhlaasw.”

Watu wataokuwa na furaha zaidi kwa sababu ya uombezi ni wapwekeshaji. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kila Mtume ana maombi yenye kuitikiwa. Maombi yangu nimeyaweka kwa ajili ya Ummah wangu siku ya Qiyaamah. Atayapata – Allaah akitaka – katika Ummah wangu yule mwenye kufa na huku hamshirikishi na Allaah na chochote.”[3]

Amebainisha (Swalla Allaahu ´alayhi w sallam) kwamba hautomfaa katika Ummah wake isipokuwa yule aliyekuwa akimpwekesha Allaah. Kuhusu yule aliyekufa katika dini nyingine mbali na Uislamu hatopata uombezi wowote. Uhakika wa mambo Allaah ndiye atatoa fadhilah Zake kuwapa watu wa Ikhlaasw na hivyo awasemehe.

Ametaja nafasi yenye kusifiwa. Ni yenye kuthibiti kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ni nafasi ambayo atasifiwa na wale wa mwanzo na wa mwisho. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَمِنَ اللَّيْلِ فَتَهَجَّدْ بِهِ نَافِلَةً لَّكَ عَسَىٰ أَن يَبْعَثَكَ رَبُّكَ مَقَامًا مَّحْمُودًا

“Na amka sehemu ya usiku na uswali ni ziada ya sunnah kwako; bila shaka Mola wako atakuinua cheo kinachosifika.” (al-Israa´ 17:79)

Cheo chenye kusifiwa ni ule uombezi mkubwa kwa mujibu wa maoni sahihi. Imesemekana vilevile kwamba nafasi yenye kusifiwa ni kwamba Allaah atamkalisha pamoja Naye juu ya ´Arshi Yake siku ya Qiyaamah. Hata hivyo usahihi wa Hadiyth hii unatakiwa kutazamwa vizuri. Maoni yanayotambulika ni yale ya kwanza.

Uombezi ni fadhilah anayopewa yule mwenye kuombewa. Ni fadhilah ya Allaah anayompa yule mwenye kuombewa ili aweze kuingia Peponi. Huu ndio uhakika wa uombezi. Hapa kuna Radd kwa waabudu makaburi. Bali wao ni wenye kunyimwa uombezi kwa sababu wanafuata ule uombezi uliokanushwa.

[1] al-Bukhaariy (7510) na Muslim (193).

[2] al-Bukhaariy (99).

[3] al-Bukhaariy (5945).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kitaab-it-Tawhiyd, uk. 63-66
  • Imechapishwa: 03/10/2018