Dada yangu muislamu! Nilikuahidi katika utangulizi ya kwamba nitakutajia ya mambo yanayoenda kinyume na Shari´ah ili uyaepuke na pia uwatahadharishe wale marafiki na wengineo wanaoyaingia. Hivi sasa ni wakati wa kuanza kuyabainisha baada ya kutaja baadhi ya nyasia na miongozo. Nasema: ee dada msafi na mwenye kujichunga na machafu:

01 – Mawasiliano ya kimapenzi

Jihadhari sana na mawasiliano yasiyokuwa ya maadili ambayo wamepewa mtihani kwayo baadhi ya vijana wa kiume na wa kike nayo. Jihadhari na mbwa-mwitu wa kibinadamu wanaokuhadaa kwa maneno matamu na misemo tamutamu kama vile: ”Ninakupenda, ee mtu wangu wa thamani sana”, ”umeuteka moyo wangu”, ”nakufikiria usiku na mchana”, ”nashindwa kulala, ”ee mwanamke mtukufu niliyemfahamu” na kadhalika. Yeye ni mwongo na mzushi. Anawajua wasichana wengine na anayasema maneno hayohayo. Hakuna kingine anachotaka isipokuwa haja yake kisha baada ya hapo akukanyage chini ya miguu yake na unakuwa kama mdoli mikononi mwake ambapo anacheza nawe vile anavotaka. Kisha akishatimiza lengo lake anakutupilia nyuma ya mgongo wake kana kwamba hajakutambua baada ya kuwa eti halali usiku na ameshakuahidi ndoa. Ghafla unasikia kuhusu ndoa yake ambapo anamuoa msichana mwenye heshima na aliyejiepusha na machafu.

Kuna kijana mmoja ambaye katika wale ambao wanawafuatilia wasichana kwenye simu kama yeye anapendelea kumuoa yule mwanamke ambaye anawasiliana naye. Akajibu kuwa hafikirii hata ile nia aliyomo na kwamba mwanamke huyo amemsaliti Mola na familia yake. Kwa ajili hiyo haaminiwi kumfanyia usaliti mume wake baada ya ndoa.

Tambua, ee dada msafi, ya kwamba wahuni hawa – namuomba Allaah asiwafanye kuwa wengi – wanakuwa na mbinu na vitimbi vingi. Miongoni mwa mbinu zao ni kwamba wanapiga simu katika nyumbani fulani na kujua ni wasichana wepi wanaoeshi humo na pengine wakati mwingine hata hawamjui msichana huyo. Badala yake wanatumia simu kama vile mbuni ya mwanzo na kumuulizia kaka yake na msichana huyo, baba yake na kuuliza ni ameenda wapi, atarejea lini, amewaelezeni nini, amewaambieni nini na anajaribu kurefusha mazungumzo. Anatumia kifaa cha kurekodia wakati wa mazungumzo. Msichana huyo atapomlegezea mazungumzo basi atampigia simu mara ya pili na mara ya tatu na hivyo ataanza kumtishia kwa kanda aliyorekodi wakati wa mazungumzo ya simu na kumwambia kuwa ataweka kanda hiyo kwenye gari la baba yake au la kaka yake. Vinginevyo yaendelee mawasiliano yetu na kweli yanaendelea na wakati huohuo anaendelea kurekodi. Kisha mwanaume huyo anamuomba wakutane ijapo karibu na mlangoni, kisha jambo linaenda mbali zaidi na hivyo anamuomba wakutane katika baadhi ya mikusanyiko ili aweze kumuona, maeneo hayo yanaweza kuwa sokoni, hospitalini na mfano wake, kisha jambo linaenda mbali zaidi na kumuomba kupanda naye usafiri mmoja na ole wake mwanamke huyo endapo atakataa. Kwani mwanaume huyo ameshakuwa na kitu cha kumtishia. Kisha anampiga picha na pengine mwanaume huyo akamuomba picha  mwanamke na kweli akampa, pengine vilevile mwanaume huyo akapiga picha akiwa pamoja naye halafu atalikaza kamatio kwa mwanamke huyo. Baada ya hapo akamuomba ambayo ni mabaya na machungu zaidi; nalo ni kule kuiporomosha heshima na utukufu wa mwanamke huyo.

  • Muhusika: Dr. ´Abdul-´Aziyz bin Daawuud al-Faaiz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tawjiyhaat wa Tanbiyhaat lil-Fataati al-Muslimah, uk. 21-23