2 – Kuamini kuwa Allaah amekiandika kila kitu kwenye Ubao uliohifadhiwa. Amesema (Ta´ala):

مَا أَصَابَ مِن مُّصِيبَةٍ فِي الْأَرْضِ وَلَا فِي أَنفُسِكُمْ إِلَّا فِي كِتَابٍ مِّن قَبْلِ أَن نَّبْرَأَهَا ۚ إِنَّ ذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ يَسِيرٌ

“Hausibu msiba wowote katika ardhi au katika nafsi zenu isipokuwa upo katika Kitabu, kabla hatujautokezesha. Hakika hayo kwa Allaah ni mepesi.”[1]

أَلَمْ تَعْلَمْ أَنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُ مَا فِي السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ ۗ إِنَّ ذَٰلِكَ فِي كِتَابٍ ۚ إِنَّ ذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ يَسِيرٌ

“Je, hujui kwamba Allaah anajua yale yote yaliyomo katika mbingu na ardhi? Hakika hayo yameandikwa katika Kitabu. Hakika hayo kwa Allaah ni mepesi.”[2]

لَا يَعْزُبُ عَنْهُ مِثْقَالُ ذَرَّةٍ فِي السَّمَاوَاتِ وَلَا فِي الْأَرْضِ وَلَا أَصْغَرُ مِن ذَٰلِكَ وَلَا أَكْبَرُ إِلَّا فِي كِتَابٍ مُّبِينٌٍ

”Hakuna kinachofichikana Kwake ingawa chenye uzito wa chembe mbinguni wala ardhini na wala kidogo zaidi kuliko hicho na wala kikubwa zaidi isipokuwa kimo katika Kitabu kinachobainisha.”[3]

Katika Hadiyth Swahiyh ambayo ameipokea Imaam Muslim kupitia kwa ´Abdullaah bin ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah ameandika makadirio ya viumbe miaka 50.000 kabla ya kuumba mbingu na ardhi na ´Arshi Yake ilikuwa juu ya maji.”[4]

[1] 57:22

[2] 22:70

[3] 34:03

[4] Muslim (2653).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Iymaan – Haqiyqatuhu wa Nawaaqidhwuh, uk. 24
  • Imechapishwa: 26/04/2023