Ni kuamini kwa kukata na kusadikisha mipango na makadirio ya Allaah. Hilo limekusanya:

1 – Kuamini kuwa Allaah aliyajua mambo kabla ya kuumbwa kwake na aliyajua yatayokuwa huko mbele. Yeye (Subhaanah) anayajua yaliyokuweko, yatayokuweko na yasiyokuweko iwapo yangelikuweko basi yangelikuwa namna gani. Amesema (Ta´ala):

إِنَّ اللَّـهَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ

“Hakika Allaah kwa kila kitu ni Mjuzi.”[1]

وَهُوَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ

“Naye juu ya kila jambo ni Mjuzi.”[2]

أَلَمْ تَعْلَمْ أَنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُ مَا فِي السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ

“Je, hujui kwamba Allaah anajua yale yote yaliyomo katika mbingu na ardhi?”[3]

عَالِمِ الْغَيْبِ ۖ لَا يَعْزُبُ عَنْهُ مِثْقَالُ ذَرَّةٍ فِي السَّمَاوَاتِ وَلَا فِي الْأَرْضِ

“Mjuzi wa mambo yaliyofichikana; hakuna kinachofichikana Kwake ingawa chenye uzito wa chembe mbinguni wala ardhini.”[4]

[1] 08:75

[2] 02:29

[3] 22:70

[4] 34:03

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Iymaan – Haqiyqatuhu wa Nawaaqidhwuh, uk. 24
  • Imechapishwa: 26/04/2023