Swali 16: Je, kitendo chake Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) kukufurisha kundi lililokataa kutoa zakaah wakati wa kupambana na wale walioasi katika waarabu baada ya kufa kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ilikuwa ni kwa sababu ya kukanusha kwao ulazima wa zakaah au kwa sababu ya kukataa tu kutoa na kutotekeleza?
Jibu: Waritadi ambao waliritadi baada ya kufa kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) walikuwa makundi mbalimbali:
1 – Miongoni mwao walirudi kwenye kuabudu masanamu na miungu na wakawaabudu.
2 – Miongoni mwao walikanusha utume wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wakiona kuwa kama angelikuwa Mtume kweli basi asingekufa, watu ambao ni makafiri bila shaka yoyote.
3 – Miongoni mwao pia walikuwepo wale waliokataa kutoa zakaah.
Maswahabah walipigana nao wote bila kuwabagua na waliwaita waritadi. Kwa wale waliokataa kutoa zakaah, wanazuoni wamesema kuwa walikufuru kwa sababu walipokataa kutoa zakaah na wakapigana kwa ajili ya jambo hilo, kitendo hicho kinafahamisha wazi kuwa walikataa ulazima wa zakaah. Hii ni kwa sababu walifanya mambo mawili:
1 – Kukataa.
2 – Kupigana kwa ajili yake.
Hata hivyo ikiwa mtu atakataa kutoa zakaah lakini asipigane kwa ajili yake, basi zakaah itachukuliwa kutoka kwake kwa nguvu na kutiwa adabu lakini hatakufurishwa. Lakini ikiwa atakataa na kupigana kwa ajili yake, basi atakufurishwa. Hiyo ni dalili ya wazi ya kukanusha kwake zakaah.
Waritadi waliokataa zakaah walifanya hivyo kwa kukataa na kupigana kwa ajili yake, jambo ambalo lilijulisha wazi kuwa wameikanusha. Ndiyo sababu Maswahabah waliwachukulia wote kuwa waritadi na wakawapiga vita bila kuwabagua. Hakuna tofauti kati ya mtu ambaye amekanusha utume wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), akaabudu masanamu au mwenye kukanusha zakaah, kwa sababu atakuwa amepinga jambo ambalo linatambulika vyema katika dini.
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: As-ilah wa Ajwibah fiy-Iymaan wal-Kufr, uk. 41-42
- Imechapishwa: 07/01/2026

Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: As-ilah wa Ajwibah fiy-Iymaan wal-Kufr, uk. 41-42
Imechapishwa: 07/01/2026
https://firqatunnajia.com/16-aina-ya-watu-walioritadi-baada-ya-kufariki-kwa-mtume/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket