Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:

Isitoshe wengi katika watu hawa wanasema kuwa maandiko haya yanatakiwa kupitshwa na kuaminiwa juu ya udhahiri wake na sambamba na hilo wanasema kuwa Allaah pekee ndiye anayejua maana yake. Huku ni kujigonga kwao. Wengi katika wale wanaojinasibisha na Sunnah, wakiwemo wafuasi wa wale madhehebu manne, wametumbukia katika jambo hili.

MAELEZO

Wanaona kuwa yanatakiwa kupitishwa juu ya dhahiri yake, kwa maana kwamba yasomwe na yapitishwe kama yalivyokuja, lakini yasifasiriwe. Nadharia yao hii inapelekea kwamba dhahiri yake ndiyo inayokusudiwa, nayo ni yale yanayofahamishwa na majina na sifa za Allaah. Kisha wanajigonga na kusema kwamba hayako juu ya dhahiri yake na kwamba yana maana ambayo haijulikani isipokuwa na Allaah. Baadhi yao wanaweza kujinasibisha na madhehebu ya maimamu wanne katika mambo ya mataga ya dini, lakini sambamba na hilo wakaenda kinyume nao katika mambo ya misingi.

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaa al-Hamawiyyah, uk. 259
  • Imechapishwa: 23/07/2026