158. Kufanana kwa Mu´attwilah na Mufawwidhwah

Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:

Tamko ya neno (التأويل) linaweza kuwa na maana tatu:

1 – Kuligeuza tamko kutoka katika uwezekano wenye nguvu na kwenda katika uwezekano usiokuwa na nguvu kwa dalili inayoelekeza hivo. Istilahi hii inatumiwa  na wengi waliokuja nyuma. Kwa mujibu wa watu hawa maana thabiti ya tamko inayoafikiana na dalili ya wazi haiwi tafsiri yoyote. Wamedhani kuwa tafsiri kama hii ndio makusudio ya Allaah pale anapozungumzia tafsiri na kwamba maandiko yanayo tafsiri inayoenda kinyume na udhahiri wake. Hakuna mwingine anayeijua isipokuwa Allaah – hata wale wafasiri hawaijui.

MAELEZO

Hii siyo maana iliyokusudiwa katika Aayah waliojengea dalili, kwa sababu ni aina mpya iliyobuniwa na watu wa baadaye. Walidhani kwamba maana iliyokusudiwa kwa tafsiri iliyokuja katika maneno ya Allaah ni hii tafsiri mpya iliyobuniwa na watu waliokuja baadaye, nayo ni kugeuza tamko kutoka katika dhahiri yake kwenda kwenye maana nyingine wanayoichagua wao. Kwa sababu Mu´attwilah na Mufawwidhwah wote walifahamu kutoka katika Maandiko maana isiyomstahiki Allaah (´Azza wa Jall). Hivyo Mu´atwwilah walizifasiri kwenda kinyume na dhahiri yake. Mufawwidhwah wao wakasema kuwa hayako juu ya dhahiri yake na hivyo wanaegemeza maana yake kwa Allaah.

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaa al-Hamawiyyah, uk. 258
  • Imechapishwa: 23/07/2026