Mtunzi wa kitabu (Rahimahu Allaah) amesema:

“… hata wakidhulumu.”

Hata kama watawala watakuwa wenye kudhulumu kwa kuchukua mali zao, qkupiga migongo yao au wakawaua waislamu, hawaoni kufaa kufanya uasi dhidi yao. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Msikilize na umtii kiongozi hata kama atakupiga mgongo wako na akachukua mali yako. Sikiliza na utii!”[1]

Ni bora kuwasikiliza kuliko kuwafanyia uasi kutokana na yale madhara makubwa yanayopatikana kwa kuwafanyia uasi. Inahusiana na kufanya kitu kidogo chenye madhara kwa ajili ya kuzuia madhara yaliyo makubwa zaidi, jambo ambalo ni moja katika kanuni za Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameamrisha kuwa na subira kwa watawala hata kama watadhulumu, wakanyanyasa na wakatenda maasi.

[1] Muslim (1847).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 171
  • Imechapishwa: 01/12/2024