Kuna watu katika walinganiaji waovu ambao wanasema msiwafunze watu Tawhiyd wala ´Aqiydah. Wanasema vijana wa waislamu wasifunzwe ´Aqiydah kwa sababu eti ni waislamu haina haja ya kuwafunza ´Aqiydah. Kwa sababu eti ni waislamu na hivyo hawahitajii kujifunza. Wanasema kuwa ni waislamu wa mjini na hivyo hawahitajii kuwafunza Tawhiyd. Je, huku si kupuuza kujifunza dini? Huku ndio kupuuza kujifunza dini. Dini haichukuliwi kwa kuirithi na kwa kuwa mtu wa mjini, dini inachukuliwa kwa elimu na kujifunza nayo. Kwa hivyo ni wajibu kujifunza dini na kuitendea kazi. Yule ambaye hajifunzi dini kwa kuipuuza na wala haitendei kazi akiwa na uwezo wa kufanya hivo, haijalishi kitu hata kama anatamka shahaadah, ni mwenye kuritadi na amefanya moja katika vichenguzi vya Uislamu. Jambo hili ni la khatari.

Kupuuza, ikiwa ni katika kujifunza mambo ya misingi ya dini na ´Aqiydah na kutoyataka, hiki ni kichengui Uislamu. Ama kupuuza ikiwa ni katika kujifunza mambo ya upambanuzi wa dini na upambanuzi  wa hukumu kwa sababu ya uvivu au kutokuwa na wakati wa kufanya hivo, haya ni maasi lakini hata hivyo haichukuliwi ni jambo linalomtoa mtu katika Uislamu. Kuhusu misingi ya dini ambayo dini ya mtu haisimami isipokuwa kwayo, haya yule mwenye kuyapuuza Uislamu wake unachenguka. Mambo ya kina hukumu za biashara na mengineyo, ni kama tulivyotangulia kutaja ya kwamba ni faradhi kwa baadhi ya watu. Katika hali watakuwa wameacha jambo lililopendekezwa na hivyo wana upungufu na kasoro kwa kutojifunza kwao hukumu kwa sababu ya kutokuwa na uchangamfu, uvivu na kutokuwa na uelewa. Kwa sababu yule mwenye kuacha kujifunza elimu ambayo ni faradhi kwa baadhi ya watu, anakuwa ameacha Sunnah na si kwamba ameacha jambo la wajibu. Ni wajibu kuyajua mambo haya na vidhibiti hivi juu ya kukengeuka na kutambua ni lini inakuwa kufuru na ni lini inakuwa madhambi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 195-196
  • Imechapishwa: 14/03/2019