154. al-´Ayyaashiy upotoshaji wake wa pili wa al-Anfaal

al-´Ayyaashiy amesema:

”Bashiyr ad-Dahhaan ameeeleza kuwa amemsikia Abu ´Abdillaah akisema: “Hakika Allaah amefaradhisha utiifu wetu ndani ya Kitabu Chake. Kwa hivyo haistahili kwa watu kutotujua. Sisi ndio wenye haki ya mali, ngawira safi za vita na utukufu ndani Qur-aan.”[1]

Allaah amemtakasa Abu ´Abdillaah kutokana na huu uzushi wa wazi. Allaah hakufaradhisha kuwatambua Mitume wote. Amesema (Ta´ala) juu yao:

وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا رُسُلًا مِّن قَبْلِكَ مِنْهُم مَّن قَصَصْنَا عَلَيْكَ وَمِنْهُم مَّن لَّمْ نَقْصُصْ عَلَيْكَ

“Hakika Tumewapeleka Mitume kabla yako; miongoni mwao wako Tuliokusimulia na miongoni mwao wako ambao hatukukusimulia.”[2]

Hivyo wale ambao Allaah ametaja ndani ya Qur-aani, basi ni wajibu kwa watu kuwaamini kwa dhati zao. Yule anayemkanusha yeyote katika wao anakufuru. Na wale ambao hakuwataja kwa majina ni wajibu kwa watu kuamini kwa ujumla.

Allaah hakufaradhisha kuwatii watu wa Nyumbani kwa njia isiyofungamana. Wale watu wa Nyumbani ambao watashika utawala wa waislamu basi ni lazima kuwatii katika mema na ni wajibu kuwaasi katika maovu. Na wale ambao hawana madaraka ya waislamu miongoni mwao ni lazima kuwatii kuwatii wale walioshika madaraka ya waislamu katika mema, hata ni muislamu mwenye kudhulumu. Haijuzu kwao kuwaasi wala kufanya uadi dhidi yao isipokuwa kama atadhihirisha kufuru ya wazi. Hili ni jambo ambalo Allaah ameliweka ndani ya Shari´ah kupitia kwa Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Basi yeyote atakayekataa hili ni miongoni mwa wapotevu, pasi na kujali ni miongoni mwa watu wa Nyumbani au mwengine yeyote.

Angalia huu usemi wa kijinga unaotokana na tamaa na hisia ya uchoyo kwa mali ya watu:

“Sisi ndio wenye haki ya mali, ngawira safi za vita… “

Naapa kwa Allaah ya kwamba hakuna anayetamka maneno haya mabaya isipokuwa Raafidhwah Baatwiniyyah. Hayakusemwa na Abu ´Abdillaah wala mwengine katika waislamu wakweli. Allaah awalaani wapotofu hawa! Ni mara ngapi wamewazulia watu wa Nyumbani na ni mara ngapi wamewachafua kwa sura kama hii yenye kudhalilisha! Yote haya ni ili wapate kula kwa kutumia jina la watu wa Nyumbani.

[1] Tafsiyr al-´Ayyaashiy (2/47).

[2] 40:78

  • Muhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 215
  • Imechapishwa: 18/02/2025