al-´Ayyaashiy amesema:
”Muhammad bin Abiy Yaziyd ar-Raaziy amesimulia kutoka kwa bwana mmoja ambaye amesimulia kutoka kwa ar-Ridhwaa ambaye amesema: “Pale mnapofikwa na shida, basi mwombeni msaada Allaah kupita kwetu. Hiyo ndio tafsiri ya maneno Yake Allaah:
وَلِلّهِ الأَسْمَاء الْحُسْنَى
”Allaah ana majina mazuri mno.”[1]
Naapa kwa Allaah kwamba sisi ndio majina mazuri ya Allaah. Hakuna matendo ya yeyote yanayokubalika isipokuwa kwa kututambua.”[2]
Allaah amemtakasa Abu ´Abdillaah na ar-Ridhwaa kutokana na uongo huu ambao hata mayahudi wanaona aibu juu yake. Je, hayakutosheni mashambulizi yenu kwa Mitume na Maswahabah kwa kuwapokonya nafasi na sifa zao? Sasa mnafikia hatua ya kuthubutu kuyashambulia majina mazuri ya Allaah na kuyahusisha kwa maimamu wanyonge ambao hawamiliki juu ya nafsi zao kuleta manufaa wala kuepusha madhara? Wajinga wanakusudia kufanya Tawassul kupitia wao kwa Allaah. Hata hivyo si jambo lililo mbali sana kwamba wanamaanisha kuwaomba msaada moja kwa moja maimamu na kuwakufurisha waislamu kwa sababu hawawatambui maimamu.
Allaah hakuwajibisa jambo hili. Allaah hatowauliza watu juu yao. Bali watu, wakiwemo maimamu, wataulizwa kuhusu kuwaamini kwao Mitume na yale waliyokuja nayo.
[1]07:180
[2] Tafsiyr al-´Ayyaashiy (2/42).
- Muhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 212
- Imechapishwa: 17/02/2025
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)