15. Zawadi ya nne: Mlinganizi anatakiwa kujipamba kwa tabia njema

Kwa njia ya kwamba ionekane ile athari ya elimu katika ´Aqiydah, ´ibaadah, sifa na katika tabia zake zote mpaka awakilishe jukumu la mlinganizi anayelingania katika dini ya Allaah. Lakini akiwa kinyume na hivo basi ulinganizi wake utafeli na endapo atafaulu basi kufaulu kwake kutakuwa kuchache sana.

Ni lazima kwa mlinganizi apambike na zile ´ibaadah, miamala na tabia anazolingania ili ulinganizi wake uwe wenye kukubaliwa na ili asiwe miongoni mwa wale wa mwanzo watakaotiwa Motoni.

Enyi ndugu! Hakika tukizitazama hali zetu basi tutaona kwamba ukweli wa mambo ni kwamba tunaweza kulingania katika kitu na wakati huohuo sisi hatukifanyi. Hapana shaka yoyote kwamba hiyo ni kasoro kubwa. Isipokuwa kama kutakuwa kuna kizuizi kati yetu sisi na kutazama kile ambacho kina manufaa zaidi. Kwa sababu kila mahali kuna maneno yake. Kitu ambacho ni bora wakati mwingine kinaweza kushindwa kutokana na sababu kadhaa ambapo kile kisichokuwa na ubora kikawa na nguvu zaidi. Kwa ajili hii Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akilingania katika baadhi ya sifa lakini wakati mwingine anashughulishwa na yaliyo muhimu zaidi. Wakati mwingine pengine akafunga mpaka watu wakasema kuwa hatofungua na mara nyingine akala mpaka watu wakasema kuwa hatofunga.

Enyi ndugu! Mimi nataka kwa kila mlinganizi ajipambe kwa tabia ambazo zinalingana na mlinganizi ili awe mlinganizi wa kweli na ili maneno yake yawe karibu zaidi katika kukubaliwa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Zaad Daa´iyah ila Allaah, uk. 21
  • Imechapishwa: 04/11/2021