Yule anayeharamisha kuchuma, biashara na kutafuta mali kutoka katika njia zake sahihi, basi amefanya ujinga na amekosea na ameenda kinyume. Bali machumo kutoka katika njia zake sahihi ni jambo la halali; Allaah (´Azza wa Jall), Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wanazuoni wa Ummah wamehalalisha mambo hayo.

Mwanamme anatakiwa kupambana kujihudumia yeye mwenyewe na familia yake. Ajipinde kutafuta riziki ya Mola wake. Ambaye ataacha kufanya hivo kwa sababu haoni kufaa kwa machumo, basi ni mwenye kwenda kinyume. Kila mmoja anayo haki ya mali yake aliyorithi, aliyoipata, aliyoachiwa wasia au aliyoichuma. Hivo ni tofauti na vile wanavosema wanafalsafa wenye kwenda kinyume.

  • Mhusika: Imaam Harb bin Ismaa´iyl al-Kirmaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-us-Sunnah, uk. 73
  • Imechapishwa: 30/05/2022