15. Swalah iliyoswaliwa kinyume na Qiblah inayotakiwa kurejewa

Swali 15: Ni ipi hukumu pale inapobainika ya kwamba swalah imeswaliwa kinyume na Qiblah baada ya mtu kujitahidi? Je, kuna tofauti ikiwa hayo yametokea katika nchi ya kiislamu au ya kikafiri au yametokea jangwani[1]?

Jibu: Ikiwa muislamu yuko safarini au katika nchi ambayo hapati wepesi wa ambaye atamwelekeza katika Qiblah, basi swalah yake ni sahihi akijitahidi katika kukitafuta Qiblah kisha ikabainika kuwa ameswali kinyume chake.

Lakini akiwa katika nchi ya kiislamu, basi swalah yake si sahihi. Kwa sababu inawezekana kumuuliza ambaye anaweza kumwelekeza Qiblah. Kama ambavo inawezekana pia kutambua Qiblah kupitia misikiti.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (10/420).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Musaafir, uk. 30
  • Imechapishwa: 01/03/2022