Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

اهْدِنَا الصِّرَاطَ الْمُسْتَقِيمَ صِرَاطَ الَّذِينَ أَنْعَمْتَ عَلَيْهِمْ غَيْرِ الْمَغْضُوبِ عَلَيْهِمْ وَلَا الضَّالِّينَ

“Tuongoze njia iliyonyooka; njia ya wale Uliowaneemesha, si ya walioghadhibikiwa wala waliopotea.”[1]

Bi maana kinyume na ile njia ya wale uliowaghadhibikia na kinyume na ile njia ya wapotofu. Watu hawatoki nje ya mafungu haya matatu:

1 – Wale walioneemeshwa ambao wanafuata njia ilionyooka na wakapita kwa mujibu wa elimu.

2 – Wale walioghadhibikiwa. Nao ni wale walioitambua elimu pasi na kuitendea kazi na wakafuata matamanio yao.

3 – Wapotofu. Ni wale wanaomwabudu Allaah kwa ujinga na hawana elimu.

Watu wako sampuli tatu:

1 – Wajuzi na watendaji; hawa ndio watu wa njia ilionyooka.

2 – Wajuzi wasiotenda. Hawa ndio walioghadhibikiwa, kwa sababu wameitambua lakini hawakuitendea kazi. Hawana udhuru.

3 – Wapotofu ambao hawarejei katika elimu. Wanamwabudu Allaah kwa mujibu wa matamanio yao, desturi zao na kufuata kwao kichwa mchunga na pasi na dalili. Wanamwabudu Allaah kwa Bid´ah, mambo yaliyozuliwa na ukhurafi ambayo shaytwaan amewapambia.

Kundi la kwanza pekee ndio limeokoka. Hayo makundi mawili mengine wako vizani. Tunamuomba Allaah atukinge dhidi ya hilo!

[1] 1:6-7

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaaa al-Hamawiyyah, uk. 41
  • Imechapishwa: 28/07/2024